Safari ya ndoto, jasho, na matumaini inafikia kilele chake! Jumapili, Aprili 19, ukumbi wa Super Dome, Masaki utashuhudia historia ikiandikwa. Mrembo mmoja kati ya 20 atatawazwa kuwa mshindi wa Miss World Tanzania 2026 na kuwa mwakilishi wa 30 wa taifa letu kwenye jukwaa la dunia nchini Vietnam! 🇻🇳
Nini kimeifanya safari hii kuwa adimu na ya kipekee?
✨ Urembo Wenye Kusudi: Chini ya nguli Mustafa Hassanali, ushindani wa mwaka huu umekuwa "moto." Majaji wapo njia panda kutokana na ubora, akili, na maono ya washiriki wote kupitia falsafa ya Beauty with a Purpose.
🚄 Kishindo cha SGR & Uzalendo: Warembo walipata fursa adimu ya kusafiri kwa SGR kwenda Dodoma, wakijionea maendeleo ya nchi na kutembelea Bunge, Mji wa Serikali, na Hospitali ya Benjamin Mkapa—wakijifunza kuwa viongozi na mabalozi wa kesho.
🏟️ Baraka za Serikali: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewapa rungu washiriki kuwa mabalozi wa heshima, utamaduni, na mshikamano wa taifa letu, kuelekea pia michuano ya AFCON 2027.
🔥 Maandalizi Makali: Kuanzia michezo (AR FITNESS), mitindo ya kiwango cha juu, hadi mafunzo ya kitaalamu ya kujipamba (Atsoko), warembo hawa wamepikwa wakapika!
🗳️ People’s Choice: Hamasa ipo juu! Kura za wananchi nchi nzima zinaamua nani ataingia Top 10 moja kwa moja. Umoja wa Watanzania umeonekana hapa!
Nani kuandika historia mpya?
Je, taji litaenda Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini, Pwani, ama ni zamu ya binti mtanashati wa Zanzibar? 🏝️
📍 WAPI: Super Dome, Masaki.
📅 LINI: Jumapili Aprili 19.
⏰ MUDA: Saa 1:30 Usiku.
Usikose kushuhudia urembo wenye kusudi ukishika hatamu! 🇹🇿✨

Comments