Yanga imezidi kutanua pengo la pointi kileleni katika Ligi Kuu Bara kufikisha nane baada ya usiku huu kuifyatua Coastal Union kwa mabao 3-0, huku Allan Okello akihusika na mabao yote.
Yanga imepata ushindi huo kwenye mechi ya Ligi iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Okello akifunga mabao mawili na kuasisti bao la tatu lililotumbukizwa na Maxi Nzengeli.
Ushindi huo ni wa 16 msimu huu kupitia mechi 22 na kufikisha pointi 54 na unbeaten ya 42 tangu ilipopoteza mechi ya mwisho Novemba 7, 2024.
Okello aliiongoza Yanga hadi mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 kabla ya kuongeza la pili kipindi cha pili na kumsetia Maxi pande safi akipokea pasi ya beki Yao Kouassi na nyota huyo Mkongomani kutupia chuma cha tatu.
Coastal licha ya kupoteza, lakini ilionyesha soka la ushindani, ila ilizidiwa na vijana wa Abdihimid Moallin anayeendeleza ubabe wa Yanga wa Wagosi kwa kuifunga mechi ya 10 mfululizo katika Ligi yangu 2021.
Okello aliyekuwa nyota wa mchezo huo ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya mechi iliyopita dhidi ya KMC amefikisha mabao matano na asisti saba kwa sasa tangu atue nchini kupitia dirisha dogo la Januari mwaka huu kutoka Vipers ya Uganda.
Kwa sasa ni zamu ya maafande wa JKT Tanzania dhidi ya Mbeya City inayopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Nini maoni yako kwa mwanzo huu wa Moallin na moto wa Okello kwa sasa.




Comments