ASKOFU GWAJIMA: VIJANA PUUZENI WANAOCHOCHEA VURUGU


 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, amewataka vijana wa Kitanzania kuwapuuza watu wanaochochea vurugu na machafuko kutoka nje ya nchi (MARIA SARUNGI NA GENGE LAKE) na badala yake kuelekeza nguvu zao katika shughuli za maendeleo na ujenzi wa taifa.


Akizungumza Jumapili itopitq katika viwanja vya Tegeta jijini Dar es Salaam, Gwajima alisema ameshangazwa na baadhi ya wanaharakati akiwemo Maria Sarungi na wenzake kwa kile alichodai kuwa ni kuhamasisha maandamano na machafuko nchini wakati wao wenyewe wanaishi nje ya Tanzania.


Alisema Tanzania imejijengea historia na heshima ya kuwa taifa la amani, umoja na mshikamano, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kulinda tunu hiyo badala ya kuruhusu migawanyiko na vurugu kuota mizizi.


"Vurugu si utamaduni wetu Watanzania. Vijana wanapaswa kuzingatia elimu, kazi, ujasiriamali na shughuli nyingine za maendeleo badala ya kufuata watu wanaowachochea kuingia katika machafuko," alisema Gwajima.


Aidha, aliwasisitiza vijana kutambua kuwa maendeleo ya taifa yanapatikana kupitia kazi, nidhamu na uzalendo, huku akieleza kuwa amani ndiyo msingi wa ustawi wa uchumi, uwekezaji na maendeleo ya kijamii.


Gwajima alisema Watanzania wanapaswa kutumia njia za kisheria na za kidemokrasia kueleza maoni yao na kutatua tofauti zozote zinazojitokeza katika jamii bila kuvuruga amani na utulivu wa nchi.


Kauli hiyo imekuja wakati ambapo kumekuwa na mijadala mbalimbali ya kisiasa ndani na nje ya nchi kuhusu mustakabali wa demokrasia, ushiriki wa wananchi katika masuala ya kitaifa na nafasi ya vijana katika mchakato wa maendeleo.


Kwa mujibu wa Gwajima, ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha nchi inaendelea kuwa kisiwa cha amani kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.


Alihitimisha kwa kuwataka wananchi kuendelea kudumisha mshikamano wa kitaifa na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama, amani na maendeleo ya Tanzania.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

BALOZI WA CHINA KUPITIA DKT. MAJULE APELEKA NEEMA KWA WANAWAKE DODOMA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA DIT KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI