Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, amewataka viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sofi kuendelea kuimarisha chama kwa kuongeza wanachama wapya, kudumisha umoja na mshikamano, pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya wananchi.
Akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake katika Kata ya Sofi, Dkt. Mdaku alisema nguvu ya CCM inatokana na umoja wa wanachama wake na ushirikiano mzuri kati ya viongozi na wananchi. Alisisitiza kuwa chama kinapaswa kuendelea kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza na kutatua changamoto zao kupitia njia halali za Serikali.
Aidha, aliwataka viongozi wa chama katika ngazi zote kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, kulinda mafanikio yaliyopatikana na kuendeleza mshikamano utakaowezesha Jimbo la Malinyi kuendelea kupiga hatua za maendeleo.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo walimshukuru Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku kwa kuendelea kuwa karibu nao, kusikiliza maoni yao na kuwahamasisha kudumisha umoja, wakieleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu katika Jimbo la Malinyi.
Comments