TAARIFA YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI NDUGU GERSON MSIGWA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YA WANANCHI – JIJINI DODOMA TAREHE 22 JULAI, 2026
1. 1.UTANGULIZI
Ndugu wanahabari -
HABARI ZA MCHANA
...... Kazi na Utu ................. Tunasonga Mbele. Awali ya yote, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kuendelea kutujalia uzima, afya njema na amani katika nchi yetu, na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo. Aidha, naomba nitumie fursa hii kuwakaribisha kwenye mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na vyombo vya habari, unaofanyika leo tarehe 22 Julai, 2026 katika Kituo cha Afya cha Ilazo hapa jijini Dodoma. Mkutano huu ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuwajulisha wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Serikali, hususan miradi ya maendeleo na hali ya utekelezaji wa mipango ya kimkakati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa Taifa.
Aidha, Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ambayo nimekuwa nikiifanya katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa shughuli na miradi ya Serikali. Katika mikutano hiyo, nimekuwa nikitembelea maeneo yanakotekelezwa miradi nikiwa nimeambatana na waandishi wa habari ili wapate fursa ya kujionea maendeleo hayo na kuyafikisha kwa wananchi kwa usahihi zaidi.
Mkutano wangu wa mwisho nilikwenda na waandishi wa habari kwenye mradi wa 1 ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda, mkoani Morogoro ili waone kazi kubwa inayoendelea kufanyika inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya maji, kilimo, nishati na uhifadhi wa mazingira nchini. Ndugu Waandishi wa Habari; Leo nimekutana nanyi hapa Kituo cha Afya cha Ilazo jijini Dodoma kwa lengo la kuwapa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali, hususan miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi wa Taifa.
Serikali imeendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwekezaji mkubwa katika sekta za kimkakati ikiwemo afya, maji, miundombinu, nishati na huduma nyingine za kijamii. Miradi hii inaendelea kutekelezwa kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma, kukuza uzalishaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji. Ndugu Waandishi wa Habari; Katika mkutano huu, nitazungumzia maeneo makuu yafuatayo:-
1. 2. 3. Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi Miradi ya kimkakati katika sekta ya afya Miradi ya Ujenzi wa Masoko
UJENZI WA MASOKO TAARIFA YA UENDESHAJI WA SOKO LA MACHINGA KWA MWAKA WA FEDHA 2025-2026.
2 Serikali kwa kuona umuhimu wa wafanyabiashara na changamoto wanazozipitia iliamua kuwawekea utaratibu ambao utawezesha kufanya biashara zao bila kupata bugudha ambapo Mnamo tarehe 13/09/2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliagiza Halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wa biashara ndogondogo (Wamachinga) kufanyia shughuli zao. Katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wilaya ulitenga eneo la Bahi Road (eneo yalipokuwa yanaegeshwa malori ya mizigo) kuanzia mzunguko wa barabara ya kwenda Singida hadi mzunguko wa barabara ya uwanja wa Ndege kwa ajili ya kujenga soko La wazi litakalotumiwa na wafanyabiashara wa biashara ndogondogo (Machinga) hapa Dodoma ambalo lilianza kujengwa Mwezi Disemba 2021.
GHARAMA ZA MRADI
Ujenzi wa soko la wazi la wamachinga Bahi Road, umegharimu kiasi cha shilingi 9,529,747,200.66/=, ikiwa shilingi 6,529,747,200.66/= ni Mapato ya Ndani, shilingi 2,500,000,000.00/= ni ruzuku kutoka Serikali Kuu na shilingi 500,000,000.00/= ni fedha za UVIKO 19. Mradi huu wa Ujenzi wa mradi wa soko la wazi la Machinga umekamilika na tayari soko limeanza kutumika na lina wafanyabiashara 2,792 mpaka sasa na pia kuna wafanyabiashara wanaotoa huduma za soko la jioni kati ya 130 hadi 176, miamala ya fedha 48, Mama Ntilie 18, eneo la Nyama choma 10 na Baa 3.
HUDUMA ZINAZOPATIKANA NDANI YA SOKO
3 Ndani ya soko la Bahi Road kuna Wafanyabiashara ambao sio wamachinga (Watoa Huduma), na hutoa huduma kwa wamachinga ambao hufanya biashara zao katika soko hili. Watoa huduma hao wamejaza mkataba na huduma hizo ni kama Huduma za kifedha (ATMs, wakala wa fedha), Huduma Baba/mama Lishe, Salon na eneo la burudani.
HUDUMA ZA KIJAMII ZILIZOPO NDANI YA SOKO Kutokana na Idadi kubwa ya watu waliopo ndani ya soko kulilazimika kuwa na huduma za kijamii kwa ajili ya wafanyabiasha na wateja watakaotembelea soko hili. Huduma hizi ni pamoja na Kituo cha Polisi, Chumba cha matibabu ya dharura, Chumba cha kunyonyeshea Watoto, Huduma ya CCTV Cameras, Huduma ya Matangazo, eneo la maegesho la magari ya binafsi na uwepo wa huduma ya vyoo.
MIFUMO MBALIMBALI ILIYOPO KURAHISISHA USIMAMIZI WA SOKO Katika soko la Machinga kumefungwa mfumo wa ulinzi wa CCTV Kamera ambao unawezesha usalama katika soko na matukio mbalimbali yanayoweza kuhatarisha usalama wa wafanyabiashara pamoja na uchafuzi wa soko.
Mfumo huu una jumla ya kamera 46 ambazo zimefungwa katika kila block, kwa sasa kamera zote zilizofungwa zinafanya kazi na mpango wa baadae ni kuongeza kamara zingine 41 ili kuwa na jumla ya 87 ambazo zitawezesha maeneo yote ya ndani na nje ya soko kuonekana kwa ufasaha.
Mfumo wa matangazo (Public Address System) umefungwa ambao unarahisisha utoaji wa taarifa mbalimbali kwa wafanyabiashara.
4 Mfumo wa Zimamoto Katika soko kuna mfumo wa maji unaojitegemea kwa ajili ya kudhibiti majanga ya moto yanayoweza kujitokeza katika soko. Mfumo huu unatumia chanzo cha maji ya kisima kilichopo katika soko (hydrants).
SEKTA YA AFYA
Serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya afya nchini kwa kupanua miundombinu ya huduma za afya, kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa, kusogeza huduma karibu na wananchi, pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia, ikiwemo Akili Unde, kwa lengo la kuharakisha utoaji wa huduma za afya.
Kwa upande wa Afya ya Msingi, Serikali imetoa jumla ya Jumla ya shilingi trilioni 1.73 zimetolewa na Serikali kwa kipindi cha mwaka 2021/22 - 2025/26 kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, kwa ajili ya ujenzi wa wa miundombinu ya afya ya msingi pamoja na ununuzi wa Vifaa Tiba.
Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na:- 1. Ujenzi na uendelezaji wa Hospitali mpya za Halmashauri 25;
2. Ukarabati wa Hospitali Kongwe 62 za Halmashauri;
3. Ujenzi wa Vituo vya Afya 564, ikijumuisha Vituo vya Tozo 234;
4. Ukamilishaji wa maboma ya Zahanati yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi 1,586;
5.Ujenzi wa majengo 87 ya kutolea huduma za dharura (EMD);
6. Ujenzi wa majengo 30 ya huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU);
7. Ujenzi wa vituo 2 kutibu magonjwa ya milipuko;
8. Ujenzi wa mitambo 21 ya kuzalisha hewa Tiba ya Oksijeni kwa ajili ya wagonjwa mahututi na Wagonjwa wa dhararua;
9. Ujenzi wa Nyumba za Watumishi 432 (270 za 3 in 1) na 162 (stand alone); 10. Ununuzi wa Magari ya kubeba Wagonjwa (ambulance) 382 na 11.
Ununuzi wa Magari ya usimamizi shirikishi 210 Aidha, katika kipindi cha Awamu ya Sita, upatikanaji wa huduma za afya umeongezeka kwa kasi ambapo Vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka 10,153 mwaka 2021/2022 hadi 13,683 kufikia mwezi Machi 2026, ikiwa ni ongezeko la vituo 3,530.
Kati ya hivyo, i. ii. iii. iv. Zahanati zimeongezeka kutoka 7,189 hadi 8,706, Vituo vya Afya kutoka 956 hadi 1,359, Hospitali kutoka 404 hadi 475 na Vituo vingine Kutoka 1,604 hadi 3,143.
HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA
Serikali pia imetoa Shilingi bilioni 242.7 kwa ununuzi wa dawa kupitia MSD, upatikanaji wa bidhaa za dawa 382 umefikia asilimia 88.8 na hivyo kuweka msingi wa kujitosheleza kwa bidhaa za afya. Kufuatia agizo la Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuimarisha uwezo wa nchi katika kuzalisha bidhaa za afya ili kufikia azma ya kujitosheleza kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2030, Serikali kupitia Wizara ya Afya tunaendelea kukiwezesha kikosi kazi maalum cha 6 Pharmaceutical Investment Acceleration Taskforce (PIAT) kwa ajili ya kuratibu, kuwezesha na kuharakisha uwekezaji wa viwanda vipya vya bidhaa za afya nchini na hivyo kurahisisha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za Serikali kununua dawa kutoka nje ya nchi.
KITUO CHA AFYA ILAZO
Kituo cha Afya Ilazo ni moja ya mifano ya Vituo vya Afya vingi vilivyojengwa na Serikali ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za afya katika ngazi zote ikiwemo ile ya chini kabisa kwa Mwananchi. Kituo hiki kinahudumia wananchi wapatao 99,743 kutoka Kata za Ipagala, Nzuguni na maeneo jirani hapa jijini Dodoma.
Kuanzishwa kwa Kituo hiki cha Afya ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wa maendeleo, hususan KOICA kupitia UNICEF.
Mradi huu ulikabidhiwa rasmi Serikalini na ulianza kutoa huduma tarehe 1 Oktoba, 2024. Gharama za ujenzi wa mradi huu zilikuwa shilingi za Kitanzania bilioni 3.32.
Aidha, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilichangia shilingi 150,000,000/= kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya ununuzi wa samani na vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na shilingi 180,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa mifumo ya mifereji ya maji ya mvua, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha ufanisi wa utoaji wa huduma.
MIUNDOMBINU YA KITUO CHA AFYA ILAZO
7 Mradi huu umehusisha ujenzi wa majengo 9 yanayowezesha utoaji wa huduma mbalimbali za afya, zikiwemo huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Wazazi lenye Chumba cha Upasuaji na huduma za kujifungua, huduma za Watoto Wachanga, huduma za Maabara, pamoja na huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH).
Vilevile, miundombinu mingine iliyojengwa ni pamoja na Chumba cha Kuhifadhi Maiti, Kitengo cha Kufulia, Mfumo wa Umeme, Vyoo vya Umma, Mfumo wa Kuhifadhi Maji, Kichomea Taka za Hospitali, Jenereta ya Dharura pamoja na Mfumo wa Uzalishaji na Usambazaji wa Oksijeni.
Pia kituo kimeweza kuanzisha huduma za Kibingwa za Kina mama, Watoto na magonjwa ya ndani ambazo hutolewa kila wiki.
MIRADI MINGINE YA MAENDELEO YA WIZARA YA AFYA
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya afya iliyogharimu Shilingi bilioni 202.96 ambazo ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 106.62 fedha za nje.
Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-
2. Mradi wa Ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la kufulia, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la kutakasia vifaa tiba, jengo la kuzalishia hewa tiba, sehemu ya kusubiria wagonjwa, jengo la mionzi, pamoja na kazi za nje na ukamilishaji wa wodi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Burigi Chato kwa fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni tano (5).
8 3. Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Mkoa wa Dodoma unatarajiwa kugharimu jumla ya Shilingi Bilioni Nane (8), ambapo shilingi bilioni sita (6) ni fedha za ndani na shilingi bilioni mbili (2) ni fedha za nje. Kwa sasa, mradi huo upo katika hatua ya usanifu wa michoro, ikijumuisha maandalizi ya michoro ya ujenzi na BOQ. 4.
MIRADI YA UIMARISHAJI WA HOSPITALI ZA RUFAA (MIUNDOMBINU)
Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika hospitali za rufaa za mikoa kwa lengo la kuboresha huduma za afya, hususan huduma za mama na mtoto, wagonjwa wa nje (OPD), wagonjwa wa ndani (IPD), huduma za mionzi, ICU, EMD pamoja na miundombinu ya damu salama. Miradi hiyo iko katika maeneo yafuatayo :-
(i) (ii) Mkoa wa Kagera - Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa hatarishi na milipuko (Isolation Center) kwa gharama ya Shilingi bilioni 5. Kisarawe – Pwani, Kisopwa (Isolation Center), - Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa hatarishi na milipuko kwa gharama ya shilingi bilioni sita (6), ambapo kwa ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 53.
(iii) Mkoa wa Tabora - Ujenzi wa hospitali maalumu ya huduma za utengamao kwa gharama ya shilingi bilioni tano (5) ambazo ni fedha za ndani.
Kwa sasa, mradi huo upo katika hatua za awali za umilikishaji wa eneo la ujenzi. (iv) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo, tunajenga jengo la huduma za Mama na Mtoto (Maternity Complex) kwa gharama ya shilingi bilioni sita (6), 9 (v) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma - Ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5, (vi) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita - Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lenye thamani ya shilingi bilioni 8.38.
Ujenzi umefikia asilimia 60. (vii) Ujenzi wa Jengo Wazazi (Maternity Complex) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa gharama ya shilingi bilioni sita (6);
(viii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi - Ujenzi wa OPD na Maternity Complex (Wing A & B) kwa shilingi bilioni tano (5); ambapo Wing A imefikia asilimia 98 na tayari inatoa huduma, huku Wing B ikiwa imefikia asilimia 58. (ix) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara – Ligula, Ujenzi wa jengo la OPD (G+1) kwa shilingi bilioni tatu (3); sakafu ya chini imefikia asilimia 85, huku awamu ya pili ikiwa kwenye hatua za manunuzi ya Mkandarasi.
(x) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara - Ujenzi wa EMD, ICU, OPD, Utawala na Mionzi kwa shilingi bilioni moja (1); ambapo jengo la mionzi limefikia asilimia 99, OPD na Utawala asilimia 98, EMD na ICU asilimia 97, na jengo la damu salama asilimia 77.
(xi) Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa – Mara. Awamu ya nne ya ujenzi imefikia asilimia 98 na kuanza kutoa huduma, huku awamu ya tano ikiwa imefikia asilimia 65. (xii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma – Maweni Awamu ya kwanza ya jengo la OPD imekamilika kwa asilimia 100, na sakafu ya chini tayari inatoa huduma. (xiii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro–Mawenzi Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto kwa shilingi bilioni mbili (2) na ujemzi umefikia asilimia 97, huku sakafu tatu tayari zikitoa huduma. 10 (xiv) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya - Ujenzi wa OPD kwa Shilingi bilioni 3.5 upo katika hatua za kumpata Mshauri Elekezi. (xv) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro - Ujenzi wa Jengo la Wazazi (Maternity Complex) kwa Shilingi bilioni saba (7) upo katika hatua ya kumpata Mshauri Elekezi. (xvi) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha – Mount Meru - Ujenzi wa Jengo la Kulaza Wagonjwa (IPD) kwa shilingi bilioni sita (6) upo katika hatua za awali za manunuzi. (xvii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza – Sekou Toure Ujenzi wa OPD Complex kwa shilingi bilioni tano (5) upo katika hatua za kumpata Mkandarasi. (xviii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Ujenzi wa Maternity Complex kwa Shilingi bilioni saba (7) upo katika hatua za manunuzi ya Mkandarasi. (xix) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto kwa shilingi bilioni 1.06 umefikia asilimia 95 na umeanza kutumika. (xx) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine, ujenzi wa Awamu ya tatu ya jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) imefikia asilimia 5, ikihusisha uwekaji wa madirisha, milango na upakaji wa rangi. (xxi) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto kwa shilingi bilioni tatu (3) umefikia asilimia 62. (xxii) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Sumbawanga, Ujenzi wa jengo la Damu Salama kwa shilingi bilioni 2.14 umefikia asilimia 67.5 11 MIRADI YA MAENDELEO YA TAASISI ZA AFYA NA HOSPITALI ZA RUFAA ZA KANDA Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati katika taasisi maalumu za afya na hospitali za rufaa za kanda kwa lengo la kuboresha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini. Miradi hiyo ni pamoja na:- 1. Taasisi ya Saratani – Ocean Road (ORCI) - Serikali imetenga Shilingi bilioni nane (8) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya:- i. Ujenzi wa Kituo cha Saratani Kanda ya Mbeya, ambapo mradi umefikia zaidi ya asilimia 40 ya utekelezaji; ii. iii. Ujenzi wa jengo la huduma za mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara – Ligula, ambapo Mkandarasi tayari amekabidhiwa mradi kwa ajili ya kuanza utekelezaji; Tumenunua na kuifunga mashine za PET/CT scan na Cyclotron, ambao umekamilika na umeanza kutoa huduma za uchunguzi wa saratani katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dar es Salaam. 2. Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) - Serikali imetenga shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya ujenzi wa kitengo cha dharura (EMD), maabara pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya huduma za katika upimaji na upasuaji wa magonjwa mbalimbali hususan ya moyo. JKCI imeimarisha Maabara ambayo ni miongoni mwa maabara kubwa na za kisasa zaidi katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa na uwezo wa kupima zaidi ya sampuli 5000 kwa saa kwa haraka na usahihi wa hali ya juu kwa wagonjwa 12 wa ndani na nje ya taasisi hiyo. Uwekezaji uliofanywa na Serikali katika wa maabara hii umeongeza ufanisi wa huduma huku ukipunguza kwa kiasi kikubwa makosa ya kibinadamu katika uchunguzi wa maabara. Maabara hii ina mifumo ya kisasa yenye uwezo wa kutambua magonjwa hata katika hatua za awali kabisa. Pia imepunguza muda wa kusubiri majibu ya vipimo kutoka saa tatu hadi saa moja tu. Mbali na utoaji wa huduma, maabara hiyo pia inatumika kama darasa hai kwa wataalamu wa afya nchini kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu. Aidha hospitali yetu ya JKCI imewekeza mfumo wa kisasa unaowezesha kufuatilia hali ya mgonjwa akiwa nyumbani kwa kutumia kifaa maalumu cha DOZEE. Teknolojia hii hutumia shuka maalumu ambalo huwekwa chini ya godoro la mgonjwa na kumwezesha daktari kufuatilia viashiria muhimu vya afya. Kifaa cha DOZEE hutoa mtetemo na kuweza kusoma shinikizo la damu, kiwango cha hewa mwilini, mapigo ya moyo, na umeme wa moyo, na iwapo kutakuwa na shida taarifa itatumwa moja kwa moja kwa daktari kupitia simu yake ya mkononi ambayo itakuwa imeunganishwa na kifaa hicho na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya ghafla vya wagonjwa pamoja na kuokoa muda wa kuwapeleka hospitalini. JKCI imeanzisha mfumo wa kisasa wa kuweka miadi kwa njia ya mtandao (online booking) ambayo ilianza kutumika mwaka 2025. Hadi sasa hospitali ya JKCI imeshahudumia wagonjwa zaidi ya 71,506. Mfumo huo unawawezesha wagonjwa kuchagua muda wa kuonana na daktari na hivyo kupunguza msongamano na muda wa kusubiri huduma. Taasisi hiyo pia imeanzisha mfumo wa usajili wa ndugu wanaotembelea wagonjwa waliolazwa (visitors management system) unaolenga kuimarisha usalama na uratibu wa huduma wodini. 13 Kadhalika JKCI imezindua kitengo kipya cha kusafisha damu (dialysis unit) kwa wagonjwa wa moyo wanaopata matatizo ya figo, hatua inayolenga kuboresha huduma za tiba jumuishi kwa wagonjwa hao. Hii ina maanisha mgonjwa wa moyo anapokuwa hospitali na akapata changamoto ya figo kushindwa kufanya kazi basi anapata huduma ya kusafisha damu hapo hapo badala ya kumtoa na kumpeleka hospitali nyingine. Kitengo hiki chenye mashine za kisasa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200, kina uwezo wa kusafisha damu kwa wagonjwa zaidi ya nane (8) kwa siku. Uanzishwaji wa kitengo hiki umetokana na ongezeko la wagonjwa wa moyo wanaokabiliwa na matatizo ya figo hali iliyokuwa ikiwalazimu kwenda kupata huduma hiyo katika hospitali nyingine. Kuanzishwa kwa kitengo hicho ni sehemu ya mpango wa JKCI wa kuhakikisha huduma zote muhimu kwa wagonjwa wa moyo zinapatikana chini ya paa moja, hatua itakayoongeza ufanisi na kurahisisha matibabu. 3. Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) - Jumla ya Shilingi bilioni 9.75 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD Complex) na ununuzi wa mashine ya Cathlab kwa huduma za moyo. Ununuzi wa mashine hiyo umekamilika, huku ujenzi wa OPD ukiwa katika hatua ya kumpata Mshauri Elekezi. 4. Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara - Serikali imetenga Shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi, ambapo mradi upo katika hatua ya kumpata Mkandarasi. 14 5. Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza – Kibong’oto,- Ujenzi wa jengo la utawala kwa thamani ya Shilingi bilioni 2 unaendelea na umefikia asilimia 70 ya utekelezaji. 6. Hospitali ya Kanda ya Ziwa – Bugando (BMC) - Jumla ya Shilingi bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya External Beam Radiation, ambapo mchakato wa kumpata mzabuni unaendelea. 7. Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili – Mirembe- Serikali imetenga Shilingi bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, eneo la mitambo ya kufulia, Duka la Dawa la Jamii, ghala pamoja na kituo cha umahiri (Centre of Excellence). Miradi hiyo ipo katika hatua za mwanzo za kumpata Mshauri Elekezi. 8. Hospitali ya Kanda ya Kaskazini – Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) - Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za tiba ya mionzi, ambapo mradi huo umefikia asilimia 98 ya utekelezaji. 9. Hospitali ya Kanda Benjamin Mkapa- Serikali imetenga shilingi bilioni 10.8 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za mionzi (Radiotherapy and Nuclear Medicine Building) pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya CTScan, ambapo shilingi bilioni 8.8 ni fedha za ndani na shilingi bilioni mbili (2) ni fedha za nje. Kwa sasa, ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 61 ya utekelezaji.
Zaidi kuhusu HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA 15 Aidha, Serikali imewekeza jumla ya shilingi bilioni 283 katika kipindi cha miaka kumi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kutoa huduma za afya zenye ubora wa kimataifa. Serikali imewekeza katika maeneo mbalimbali muhimu, ikiwa ni pamoja na: • Ujenzi wa majengo ya kisasa ya kutolea huduma za kibingwa na ubingwa bobezi. • Ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa vinavyokidhi viwango vya kimataifa. • Kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali. • Kuboresha mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma. • Kuongeza idadi ya wataalamu wa afya na kuboresha mazingira ya kazi. • Kutokana na uwekezaji huo, Hospitali imeongezeka kutoka watumishi 20 mwaka 2015 hadi watumishi 1,076 mwaka 2026, wakiwemo zaidi ya madaktari bingwa na bingwa bobezi 100 na hivyo kuimarisha huduma huduma za kibingwa zikiwemo huduma 20 za Kibingwa na huduma 18 za Ubingwa Bobezi. Baadhi ya huduma ambazo zimeanzishwa kutokana na uwekezaji huo ni: • Upandikizaji wa Figo; • Upandikizaji wa Uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa Selimundu; • Upasuaji wa Moyo kwa Kufungua Kifua; • Uchunguzi wa Mishipa ya Moyo (Cardiac Catheterization); • Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo. • Upasuaji kwa njia ya matundu madogo (Minimal Invasive Surgery); • Ubadilishaji wa Nyonga na Magoti; • Radiolojia ya Kisasa; 16 • Uchujaji Damu (Dialysis). Huduma hizi zimepunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya wagonjwa waliokuwa wakisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu na zimeokoa fedha nyingi za Serikali na wananchi na pia kuwa kivutio cha wagonjwa kutoka nje ambapo Wagonjwa 2,897 kutoka Burundi wamehudumiwa, Wagonjwa 526 kutoka Comoro wamehudumiwa na Wagonjwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati wameendelea kupata huduma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa. Aidha, Hospitali imeanzisha Royal International Clinic, ambalo tangu kuanzishwa kwake tarehe 10 Julai 2025 tayari imehudumia wagonjwa zaidi ya 18,607, wakiwemo wagonjwa 390 wa kimataifa, pamoja na kutoa huduma za Master Health Check-up, hatua inayozidi kuiweka Tanzania katika ramani ya utalii wa matibabu duniani. Miradi Mikubwa ya Kimkakati Serikali inaendelea kuwekeza Hospitali ya Benjamin Mkapa katika miradi mikubwa itakayobadilisha sekta ya afya nchini, ikiwemo: • Ujenzi wa Jengo la Saratani lenye thamani ya shilingi bilioni 32. • Ujenzi wa Jengo la Matibabu ya Figo lenye thamani ya shilingi bilioni 44.9, ambapo Serikali ya Tanzania imechangia shilingi bilioni 16.9 na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) imechangia shilingi bilioni 28. 17 • Kuanzishwa kwa Kituo cha Umahili cha Upandikizaji Uloto. • Kuanzishwa kwa Chuo cha Afya cha Hospitali ya Benjamin Mkapa kitakachotoa mafunzo ngazi ya Diploma. Dira ya Miaka Kumi Ijayo Katika kipindi cha miaka kumi ijayo, Hospitali inalenga kujijenga kuwa Kijiji cha Utalii wa Matibabu (Medical Tourism Village) katika Makao Makuu ya Nchi, Dodoma. Dira hii inalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika kwa kuvutia wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi, kuongeza mapato ya taifa kupitia utalii wa matibabu, na kuendelea kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi. Kwa ujumla, uwekezaji wa Serikali wenye thamani ya shilingi bilioni 283 umebadilisha Hospitali ya Benjamin Mkapa kutoka hospitali mpya iliyoanzishwa mwaka 2015, kuwa kituo cha kisasa cha ubingwa kinachotoa huduma za kiwango cha kimataifa. Uwekezaji huu umeongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa, umeokoa maisha ya maelfu ya Watanzania, umepunguza gharama za matibabu nje ya nchi na umeweka msingi imara wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii wa matibabu katika ukanda wa Afrika. Maeneo mengine ambayo Serikali ipo mbioni kuwekeza katika sekta ya afya ni; 10. Hospitali ya Kanda Kigoma - Jumla ya shilingi bilioni nane (8) zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD Complex), ambapo mradi upo katika hatua za manunuzi ya kumpata Mkandarasi. 18 11. Hospitali ya Taifa Muhimbili - Serikali imetenga shilingi bilioni 61.43 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa kuhuisha ujenzi wa hospitali (Muhimbili Redevelopment Project) pamoja na ujenzi wa wodi binafsi. Kwa sasa upembuzi yakinifu umekamilika na mkataba wa ujenzi uko tayari kwa kuanza utekelezaji. 12. Taasisi ya CCBRT - Jumla ya Shilingi bilioni 1.8 zimeombwa Hazina kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vifaa tiba ili kuboresha utoaji wa huduma za afya. 13. 13.Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI) - Serikali imetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) na jengo la upasuaji pamoja na ununuzi wa vifaa tiba (Implants). Kwa sasa, ukarabati wa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) umefikia asilimia 36, huku maombi ya ununuzi wa vipandikizi yakiwa yamewasilishwa Hazina kwa ajili ya utekelezaji. Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kutekeleza miradi ya kimkakati, uboreshaji wa Miundombinu, vifaa tiba vya kisasa na kuwajengea uwezo wataalamu kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wananchi wa Tanzania pamoja na wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali.
A. MIRADI YA KIMKAKATI UJENZI WA JENGO JIPYA LA WAGONJWA WA NJE – MOI NEW OPD
Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa Jengo Jipya la Wagonjwa wa Nje la MOI wenye thamani ya shilingi bilioni 13.7. Jengo hilo litakuwa na: 19 • Vyumba 45 vya madaktari kwa ajili ya Kliniki za madaktari bingwa wa tiba ya mifupa na madaktari bingwa wa mishipa fahamu na ubongo; • Vyumba 10 vya kisasa kwa ajili ya upasuaji; • Huduma za mazoezi tiba; na • Huduma maalum za tiba kwa wanamichezo. Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 55. Kukamilika kwake kutasaidia mambo mawili; • Kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za kibingwa na bingwa bobezi • Kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaofika MOI kupata huduma • Kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma za tiba ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu
UKARABATI WA MOI ANNEX (ILIYOKUWA HOSPITALI YA TUMAINI) – UPANGA
Serikali inaendelea na ukarabati wa MOI Annex, iliyokuwa Hospitali ya Tumaini, Upanga jijini Dar es Salaam. Ukarabati huo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 2.1 na umekamilika kwa asilimia 98. Kwa sasa maboresho madogo madogo yapo katika hatua za mwisho. Serikali imefanya ukarabati huo ili kuiwezesha MOI kuweza kutoa huduma zifuatazo kwa Wananchi: • Huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika huduma za mifupa, mishipa ya fahamu na ubongo kwa wagonjwa wa nje; • Huduma kwa wagonjwa maalum; • Huduma kwa wagonjwa wa kimataifa;
20 KUIMARISHA TIBA UTALII MOI
imeendelea kupokea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika wanaofika kupata huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu. Miongoni mwa nchi ambazo wagonjwa wake wamekuwa wakipata huduma MOI ni: • Comoro; • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; • Malawi; • Msumbiji; • Sudan Kusini; • Zambia; • Burundi; • Uganda; na • Mataifa mengine jirani. Katika kipindi cha mwaka mmoja, MOI imepokea wagonjwa 270 kutoka nje ya Tanzania. Ongezeko la wagonjwa wa kimataifa linaonesha kuimarika kwa uwezo wa Tanzania katika kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa viwango vya kimataifa.
VYUMBA VYA KISASA KWA WAGONJWA MAALUM 21
Katika kuimarisha uwezo wa kuhudumia wagonjwa maalum, tiba utalii na maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027, Serikali imeiwezesha MOI kuboresha jumla ya vyumba 25 vya kisasa vya kulaza wagonjwa vyenye hadhi maalum. Vyumba hivyo vimeandaliwa kwa ajili ya: • Wagonjwa maalum kutoka ndani na nje ya Nchi • Wagonjwa wa kimataifa; • Wageni wanaohitaji huduma za kiwango cha juu; na • Wagonjwa wanaohitaji mazingira yenye faragha Maboresho hayo yataongeza uwezo wa Taasisi kuhudumia wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi.
UWEKEZAJI KATIKA VIFAA TIBA VYA KISASA i. MTAMBO WA CATH LAB KWENYE CHUMBA CHA (ANGIO SUITE)
Serikali imewekeza jumla ya shilingi bilioni 10.1 kwa ajili ya MOI kuweza kununua na kufunga mtambo wa kisasa wa uchunguzi na tiba ya mishipa ya damu kwenye ubongo bila kufungua fuvu la kichwa, unaojulikana kama Angio Suite. Mtambo huo umeleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kwenye ubongo. Kwa kutumia mtambo huo MOI sasa inaweza kufanya yafuatayo; • Uchunguzi wa mishipa ya damu kwenye ubongo; • Matibabu ya baadhi ya wagonjwa wa kiharusi; • Matibabu ya mishipa iliyoziba; 22 • Matibabu ya mishipa iliyopasuka; na • Matibabu ya vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo. Huduma hizi zote zilikuwa zinapatikana nje ya Nchi lakini kwa sasa zinapatikana hapa Nchini katika Taasisi ya MOI ii. ii.DARUBINI YA KISASA YA UPASUAJI WA UBONGO NA MGONGO MOI ina darubini ya kisasa inayotumika katika upasuaji wa ubongo na mgongo. Darubini hiyo inawawezesha wataalamu kuona kwa usahihi mkubwa sehemu ndogo na nyeti za ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu na mishipa ya damu wakati wa upasuaji. Kifaa hicho ni sawa na vifaa vinavyotumika katika hospitali kubwa duniani na kina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja (1). MFUMO WA BRAINLAB Serikali kupitia MOI imewekeza katika mfumo wa kisasa wa upasuaji wa ubongo na mgongo unaojulikana kama Brainlab, wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800. Mfumo huo unatumia teknolojia ya kisasa inayowaongoza wataalamu kutambua kwa usahihi eneo linalopaswa kufanyiwa upasuaji kwa kutumia akili unde. Brainlab husaidia: • Kuongeza usahihi wa upasuaji; • Kupunguza madhara kwa maeneo yasiyolengwa; • Kupunguza ukubwa wa sehemu inayofunguliwa; • Kuongeza usalama wa mgonjwa; na 23 • Kuboresha matokeo ya matibabu. MITAMBO YA ARTHROSCOPIC TOWERS Serikali imewekeza katika mitambo maalum ya upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu, inayojulikana kama Arthroscopic Towers. Mitambo hiyo hutumika kwa matibabu ya: • Majeraha ya magoti; • Majeraha ya mabega; • Mishipa iliyochanika; • Matatizo ya viungo kwa wanamichezo; na • Wagonjwa wengine wenye changamoto za magoti na mabega. Mtambo mmoja una thamani ya shilingi milioni 500. MASHINE ZA ULTRASOUND NA X-RAY MOI pia imeendelea kuimarishwa kwa mashine za kisasa za Ultrasound na X-ray. Mashine hizo zinasaidia katika: • Uchunguzi wa majeraha; • Uchunguzi wa mifupa iliyovunjika; • Uchunguzi wa viungo; • Kuongoza baadhi ya taratibu za matibabu; na • Kufuatilia maendeleo ya mgonjwa. 24 HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI ZINAZOTOLEWA MOI Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika vifaa tiba, wataalamu na miundombinu, MOI imeendelea kutoa huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi. • HUDUMA ZA UPASUAJI WA MIFUPA NA VIUNGO Huduma zinazotolewa ni pamoja na: • Upasuaji wa kubadilisha kiungo cha nyonga; • Upasuaji wa kubadilisha kiungo cha goti;
• Upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda; • Upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu;
• Upasuaji wa mabega kwa njia ya matundu;
• Upasuaji rekebishi wa viungo vilivyopooza; na • Tiba maalum kwa majeraha ya wanamichezo.
• HUDUMA ZA UPASUAJI WA UBONGO NA MGONGO
MOI inatoa huduma zifuatazo: • Upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu; • Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo; 25 • Upasuaji wa kuondoa uvimbe kupitia tundu la pua; • Upasuaji wa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo; • Upasuaji wa ubongo kwa kutumia mawimbi ya sauti; • Matibabu ya mishipa ya damu kwenye ubongo; • Uchukuaji wa sampuli za vipimo bila kufungua eneo kubwa; na • Uwekaji wa simenti maalum katika pingili za mgongo zilizovunjika. •
UTENGENEZAJI WA VIUNGO BANDIA KWA TEKNOLOJIA YA KISASA MOI
imeendelea kutumia teknolojia ya kisasa katika utengenezaji wa viungo bandia. Huduma hizo ni pamoja na: • Utengenezaji wa viungo bandia kwa kutumia teknolojia ya uchapishaji wa 3D; •
Utengenezaji wa mikono ya umeme; • Utengenezaji wa vifaa vya kusaidia wagonjwa kutembea; na • Utengenezaji wa vifaa maalum vinavyolingana na mahitaji ya mgonjwa. HITIMISHO - MOI Kwa ujumla, uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) umeendelea kuimarisha uwezo wa Taasisi kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Utekelezaji wa miradi ya kimkakati, 26 ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa, uboreshaji wa miundombinu pamoja na kuendelezwa kwa rasilimali watu umeongeza upatikanaji, ubora na usalama wa huduma kwa wananchi wa Tanzania na wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali. Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na mahali walipo, kupunguza rufaa za matibabu nje ya nchi, kuimarisha tiba utalii na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

Comments