BAADA ya kupata wito kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kulitumikia Taifa kupitia uteuzi wa kuwa Mkuu wa Wilaya Arumeru, Neema Lugangira ameamua kusitisha mkataba wake wa kazi wa Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Wanawake Viongozi Duniani linalojumuisha Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Wabunge Duniani (Women Political
Leaders)
Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Oktoba 3, 2026 jijini Arusha, Lugangira amesema kuwa amepokea dhamana aliyopewa na Rais Samia kwa unyeyekevu mkubwa na yuko tayari kushirikiana na wananchi na viongozi wote kuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa.
"Nimeupokea kwa unyenyekevu mkubwa uteuzi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa DC Arumeru. Kwa hatua hiyo, nimeomba ofisi yangu iliyopo Brussels nchini Ubelgiji kukatisha mkataba wangu wa Katibu Mkuu WPL, na nimerejea nchini na kuanza kazi."
"Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii. Pia namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa uteuzi alionipatia wa kumsaidia kwenye wilaya yetu ya Arumeru, " amesema Lugangira.
Amesema dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wa Arumeru wanapata viongozi wanaowasilikiza, wanaowafikia na wanachukua hatua katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Comments