
![]() |
Jana tarehe 03 Oktoba 2026, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu Zanzibar, nimetangaza uteuzi na uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, pamoja na mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara.Mabadiliko haya ni sehemu ya kukamilisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kwa kuwajumuisha Mawaziri kutoka ACT-Wazalendo, sambamba na kuendelea kutekeleza makubaliano ya maridhiano baina ya CCM na ACT-Wazalendo.
Katika uteuzi huo,
ACT-Wazalendo imepata nafasi nne za uwaziri:
• Mhe. Nassor Ahmed Mazrui – Waziri wa Afya.
• Mhe. Omar Said Shaaban – Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
• Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar – Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
• Mhe. Dkt. Mohamed Ali Suleiman – Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu.
Aidha, nimefanya mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara, ikiwemo kuhamishia masuala ya Mipango katika Ofisi ya Rais, Ikulu, pamoja na kuanzisha Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Katika mabadiliko hayo:
• Mhe. Shaaban Ali Othman – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Mipango na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.
• Mhe. Masoud Ali Mohamed – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Uhusiano wa Jamii.
• Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga – Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
• Mhe. Ali Suleiman Ameir Mrembo – Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Pia, nimefanya mabadiliko katika nafasi za Naibu Mawaziri katika Wizara mbalimbali, ikiwemo Afya, Kilimo, Elimu, Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Fedha, Utalii na Mambo ya Kale, pamoja na Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Mabadiliko haya yana lengo la kuimarisha ufanisi wa Serikali na kuendelea kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya maridhiano yaliyofikiwa baina ya CCM na ACT-Wazalendo katika uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mawaziri na Naibu Mawaziri wote walioteuliwa na waliohamishwa wataapishwa Jumatatu, tarehe 05 Oktoba 2026, saa 8:00 mchana.
Tunaendelea kujenga Zanzibar yenye umoja, utulivu na maendeleo kwa wote.





Comments