SIKU YA MIGOMBA DUNIANI-KAGERA
Mkuuu wa mkoa wa
Kagera Mheshimiwa Massawe akisikiliza maelezo kutoka kwa Wataalam wa migomba
kwenye shamba la migomba la Mubuhenge Mugoma Wilayani Ngara
Hizo ni ndizi aina
ya PHIA unaweza kujionea zinavyostawi katika Mkoa wa Kagera
Mhe. Massawe
Akitembelea mabanda kujionea wajasiliamali wanavyonufaika na zao la ndizi kwa
kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na ndizi. Chanzo; Bukoba Wadau Blog
MKOA WA KAGERA WAANZISHA SIKU YA MIGOMBA DUNIANI BAADA YA MIAKA 750 TANGU ZAO LA MGOMBA KUWEPO DUNIANI
Mkoa
wa Kagera waasisi siku ya migomba duniani tangu zao la mgomba kuwepo hapa
duniani zaidi miaka 750 iliyopita. Siku hiyo ya migomba duniani imeadhimishwa
kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Kagera Kijiji cha Rusumo na Kata
ya Rusumo Tarafa ya Nyamiaga Wilayani Ngara tarehe 19/4/2012 na
kuhudhuriwa na wakulima wa ndizi kutoka mkoa mzima wa Kagera na Wilaya ya
Kibondo Mkoani Kigoma.
Mgeni
rasmi siku hiyo ya Migomba duniani alikuwa Mhe.Kanali Mstaafu Fabian I. Masswe
pia nchi wafadhili wa kilimo cha migomba ya kisasa Ubelgiji iliwakilishwa na
Prof. Swinenon ambaye ndiye mvumbuzi wa migomba ya kisasa ya PHIA
ambayo kwasasa inastawi vizuri Mkoani Kagera na Wilayani Kibondo Mkoani
Kigoma.
Mratibu
wa mradi wa migomba Kagera Mugenzi Byachwezi aliwashukuru serikali ya Ubelgiji
inayoongozwa na mfalme kwa kufadhili mradi wa migomba Kagera kwa zaidi ya
bilioni 120 fedha za Tanzania tangu mradi ulipoanza mwaka 2009 mpaka sasa.
Aidha
Bw. Byabachwezi aliiomba serikali ya ubelgiji kuendelea kufadhili mradi huo
baada ya muda wa mradi kumalizika mwaka 2013 ili kumalizia baadhi
ya vipengere vya mradi ambavyo vitakuwa havijakamilika kwa muda huo, mfano;
kuanzisha kituo cha taarifa mbalimbali za kilimo cha mgomba mkoani
Kagera.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe katika hotuba yake aliwaomba
mradi
wa
migomba kuanza kusistiza zaidi uzalishaji wa ndizi kwa wakulima lakini pia na
kuendelea kusambaza mbegu bora za migomba. Pia kuendeleza kutoa
elimu juu ugonjwa wa migomba uitwao unyanjano unaoishambulia migomba na bado
haujapata dawa.
Pia
Mhe. Massawe aliwasistiza wananchi kuendeleza kilimo cha ndizi na kuzalisha
ndizi kwa wingi kwa ajil ya chakula na biashara na kuacha kilimo
cha kuchumia tumbo. Aidha aliwahakikishia wakulima kuwa serikali inafanya juhudi
za kutafuta masoko kutoka sehemu mbalimbali duniani ili zao la ndizi lipate bei
nzuri itayomkombao mkulima.
Mwisho
Mhe. Massawe aliishukuru serikali ya Ubelgiji kuuona mkoa wa Kagera na
kuupa
ufadhili
katika kilimo cha migomba ili kuinua kipato cha wananchi wake. Pia aliwashukuru
viongozi wa mradi wa migomba Kagera kumkaribisha
kuwa mgeni rasmi na yeye kuwa muasisi wa siku ya migomba duniani,
“Nimevunja rekodi ya dunia na rekodi yangu mwenyewe kwa kuasisi siku ya migomba
duniani.” Alimalizia Mhe. Massawe.
Siku
hiyo ya migomba Duniania iliambatana na kutembelea mashamba ya kuzalisha mbegu
na kusambaza, pia mshamba ya kuzalisha ndizi Wilayani Ngara. Aidha
wakulima kutoka kila wilaya katika mkoa wa Kagera waliweza kuonyesha bidhaa
mbalimbali zinazotokania na zao la ndizi. Pia wakulima na wajasiliamali walipewa
elimu juu ya kudhibiti ugonjwa wa unyanjano katika mashamba yao ya
ndizi.
Na:
Sylvester Raphael,
Afisa
Habari Mkoa,
KAGERA
Comments