WIZARA YA AFYA NA USTAWAI WA JAMII YAFANIKIWA KUAJIRI WATUMISHI 27,795 KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2005/2013.
Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Nsachris Mwamwaja akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu
Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Nsachris Mwamwaja (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM).Kushoto ni Afisa Ustawi
Mwandamizi Mkuu kutoka kutoka Wizara hiyo, Josephine Lyengi na Kulia ni Afisa Habari
wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi. Picha
zote na Georgina Misama-MAELEZO
=========== ========== ========
Na Frank Mvungi
WIZARA ya Afya
na Ustawi wa jamii imefanikiwa kuajiri watumishi 27,795 katika kipindi cha
mwaka 2005/2013.
Hayo yamesemwa
na Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Nsachris wakati
wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam wakati akizungumzia
mafanilkio ya mpango wa maendeleo ya Afya ya msingi (MMAM).
Mwamaja
amebainisha kuwa lengo kuu la mpango huo ni kusogeza huduma za afya ya msingi
kwa wananchi wote kwa ubora unaokubalika karibu zaidi na wanakoishi. Alisema aidha
malengo mahususi ya mpango wa MMAM ni
kuongeza, kurekebisha, kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya na ustawi wa jamii na kuhakikisha
huduma zinatolewa kwa usawa na kuwafikia wananchi wote.
Aliongeza kuwa
mpango huo unalenga kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu, vifaa tiba na
dawa zenye ubora katika vituo vya afya ili kuhakikisha utendaji ulio bora. Mwamwaja
aliongeza kuwa ni vyema wananchi
wakashiriki katika kuhakikisha kuwa mfumo huo unafanya kazi ili kuleta
tija na kufikiwa kwa malengo ya mpango huo.
Katika mpango
huo wa MMAM, Serikali imeongeza udahili kwa wanafunzi wa wanaosoma kada za Afya
nchini kwa mwaka 2012/2013 hadi kufikia
7,956. Mwamaja aliongeza
kuwa Wizara ya Afya imepewa kibali cha
kuwapangia vituo vya kazi watumishi 11,221 wa kada za afya ambapo zoezi hilo linaendelea.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miongozo ya Kitaifa na Kimataifa ikiwemo Dira ya Taifa 2015, MKUKUTA II, malengo ya millennia,Ilani ya uchaguzi na sera ya Taifa ya Afya.
Comments