Nikiwa ndani ya treni hiyo ya SGR. KWANZA kabisa napenda kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya ujenzi wa treni ya kisasa ya umeme maarufu SGR ambayo imeanza kufanya kazi mwaka jana wa 2024, hivyo kurahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam- Morogoro na Dodoma. Usafiri huo wa SGR umepokelewa na wananchi kwa mikono miwili, kwani kila siku tangu uanze umekuwa ukijaa abiria wanaoenda maeneo mbalimbali ya nchi. Ukipanda SGR kuna raha yake; haichoshi kutokana na muda mchache inaotumia, ina usalama zaidi tofauti na usafiri wa barabara, haina mitikisiko, huduma safi ya vinywaji na vitafunwa, huduma ya choo, luninga bila kusahau kiyoyozi na kusikia sauti nyororo ya Binti ikitangaza kila kituo cha kupanda na kushuka pamoja na huduma zi...
Comments