Ratiba ya mazishi ya Linah Harrison Mwakyembe imetolewa na familia ambapo inaonesha kuwa Jumanne, Julai 18 shughuli za mazishi zinatarajiwa kuanza rasmi asubuhi nyumbani kwa Dk. Harrison Mwakyembe, Kunduchi Beach na marehemu ataagwa katika kanisa la Usharika wa KKKT Kunduchi jijini Dar es salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana. Marehemu anatarajiwa kusafirishwa kwa ndege hadi mkoani Mbeya ambako anatarajiwa kuzikwa Jumatano Julai 19, 2017.
CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO
Chama cha Kulinda na Kuwatetea Walimu Tanzania (CHAKUWAHATA) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata la baadhi ya wakurugenzi kukiuka sheria ya kuwaruhusu walimu kujiunga na chama hicho hivyo makato ya fedha za mishahara yao kuingizwa kwenye chama hicho. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Herman alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wao unaofanyika jijini Dodoma. Walimu ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kupitia upya rasimu ya katiba ili ieendane na wakati.
Comments