SILLO AISHAURI SERIKALI KUIWEZESHA TRA IWE NA MIFUMO MIZURI YA UKUSANYAJI KODI+video

 


Mbunge wa Babati Vijijini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuongeza mafunzo kwa walipa kodi nchini ili kuongeza wigo wa kukusanya kodi.

Aidha, Sillo ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango kuongeza mafunzo kwa wakaguzi wa kodi za ndani, pia waiwezeshe TRA kuwa na mifumo ya kisasa ya kukusanya kodi. Ametoa ushauri wake huo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo bungeni Dodoma Juni 7,2022.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Sillo akitoa ushauri wake huo....


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO TV/BLOG
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO

JINSI YA KUMTAWALA MWANAMKE HASA MKE (USIOE MKE WA MTU)

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI

MWANDISHI WA HABARI SAGGAF ACHUKUA FOMU ZA UBU/NGE DODOMA MJINI