Gloria, ambaye anasoma katika Chuo Kikuu cha Cornell nchini Marekani na tayari ana shahada mbili, aliibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2025/2026 baada ya kuwashinda washiriki zaidi ya 1,000 kutoka mataifa mbalimbali. Ushindi huo ulimwezesha kutembea kwenye zulia jekundu (Red Carpet) kama sehemu ya hafla ya utoaji wa tuzo.
Kupitia mafanikio hayo, Gloria ameendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa. Mabango yanayotangaza ushindi wake na filamu hiyo yamewekwa katika maeneo mbalimbali jijini New York, Marekani.
Filamu hiyo, inayoangazia ugonjwa wa malaria ambao unaendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwemo Tanzania, imepata umaarufu mkubwa nchini Marekani na kuvutia watazamaji wengi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Gloria ameandika historia kwa kuwa Mwafrika wa pili kushinda tuzo hiyo ya kimataifa ya uandishi wa filamu.



Comments