MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:
Katika Mambo haya Hakuna yametofautiana kutokana na aina ya maisha mnayoishi na mumeo lakini wanaume wengi wapo hivi. 1__.MWANAMUME HAPENDI KUFOKEWA: Hata Kama amekosea; jaribu kumuonyesha kosa lake pasipo kumfokea au kumvunjia heshima. 2__ MWANAMUME HAPENDI KUULIZWA MASWALI MENGI KWA WAKATI MMOJA: Ukimuuliza swali halafu yeye anakua kimya au anaduwaa; ujue hana jibu au anajisikia vibaya kuhusu jibu ambalo anatakiwa kutoa. Mpe muda ajipange kutoa jibu usimlazimishe siyo mtumwa wako. 3__ MWANAMUME ANAHITAJI MUDA WA KUKAA KIMYA; USIMLAZIMISHE KUONGEA: Zaidi sana anapopita kwenye hali ngumu au changamoto fulani; wanaume wengi hupenda kukaa kimya huku akiwaza nini cha kufanya. Tofauti na wanawake, ambao wakati wa changamoto ndipo wanataka kuongea zaidi. Wanaume wengi hawapendi kuongea kama hawana suluhisho la shida iliyopo mbele yao hivyo Kama wewe ni mtu sahihi kwake jifunze kumsoma mumeo ili ujue nyakati zake ngumu ili usimame kwenye zamu yako. 4__ MWANAMUME ...
Comments