HATUTASHIKA DOLA KWA MABAVU WALA BUNDUKI- GAVU

 


> _Awataka wana CCM kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa kutuma salamu za ushindi mkubwa kwa Rais Samia katika uchaguzi wa mwaka 2025_ 


Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndugu. Issa Haji Gavu , amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kama ilivyo kawaida yake kamwe hakitashika dola kwa mabavu wala kutumia bunduki bali kitashika dola kwa hila ya kidemokrasia.


Ndugu. Gavu ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano uliokutanisha Viongozi wa Chama, Serikali, Taaisis ziziso za kiserikali, Viongozi wa Dini, Wazee na Machifu.


"Hatutashika dola kwa mabavu wala bunduki bali tutashika dola kwa hila za kidemokrasia"


"Msingi wa demokrasia ni kupiga kura, ili mwanadamu ashawishike basi una wajibu wa kumshawishi kabla ya kupiga kura"


"Tuhakikishe tunaendelea kuhamasisha na kuchapa kazi kwakuwa ndio kitu pekee kitakachoendelea kutupa thamani kwa wananchi kuendelea kutuamini"


"Tutumie uchaguzi wa serikali za mitaa kama salamu za ushindi atakaokwenda kuupta Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ifikapo mwaka 2025"


πŸ—“️16 Aprili, 2024

πŸ“Mbozi - Mkoani Songwe


#CCMKazini

#VitendoVinaSauti

#TuaendeleaNaMama

#KaziIendelee


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI