MFUMO WA KIDIJITALI WA KUTOA BARUA YA UTAMBULISHO WA MKAZI WAZINDULIWA



 Na John Banda, Dodoma

KATIBU mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla  amezindua mfumo wa Anwani za Makazi utakaowawezesha wananchi kupata barua za utamburisho kupitia simu zao za mikononi.

Katika Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dodoma, Aprili 16,2024 umeambatana na uagawaji wa Kompyuta na Vishikwambi vitakavyotumiwa na watendaji wa kata na mitaa kwa baadhi ya halmashauri hapa nchini kwa ajili ya majaribio ya miazi mitatu huku serikali  ikiahidi kugawa vitendea kazi hivyo kwenye kata zote 4,066 hapa nchini baada ya majaribio hayo

Akiongea Katika uzinduzi huo Katibu Mkuu huyo amesema kuanzisha mfumo wa anuani za makazi ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003; makubaliano ya Kikanda kupitia Umoja wa Posta Afrika yaani Pan Africa Postal Union -PAPU; makubaliano ya Kimataifa kupitia Umoja wa Posta Duniani yaani Universal Postal Union - UPU; na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya miaka mitano, 2020 – 2025.

Amesema Kwa lugha rahisi, NAPA ni daftari la kidijitali la ukazi ambalo linawezesha Serikali Kuu, Serikali za Mtaa/kata au Shehia pamoja na mambo mengine kujua Idadi wa Watu walio kwenye eneo husika hivyo urahisi wa kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia uhalisia wa watu na huduma zilizopo katika eneo husika.   

Ametabaisha kuwa mfumo huo utamuwezesha Mwananchi kuweza kuomba anwani kijiditali. Aidha, mwananchi anaweza kuomba kuhamisha anwani yake anayoishi kutoka sehemu moja kwenye nyingine kupitia simu ya mkononi bila hitaji la kwenda Serikali za Mtaa huku ukiwawezesha Watendaji wa mitaa/shehia/vijiji kushughulikia maombi ya wananchi kwenye mfumo wa NAPA kwa kutumia simu au vishwambi.

Ameongeza kuwa Wizara itahakikisha kuwa vishikwambi vinavyogawiwa vinakuwa na intaneti hivyo watendaji hawataingia gharama za ununuzi wa Bando kwa muda wote wa kipindi cha majaribio ili waweze  kumhudumia mwanananchi bila kikwazo chochote cha kimfumo.

“Majaribio haya yatakuwa ya muda wa Miezi Mitatu na baada ya hapo Wizara itafanya tathmini na kuboresha kulingana na matokeo ya tathmini husika” amesema

Aidha amesema  Baada ya hapo utafanyika uzinduzi rasmi wa Mfumo ili uweze kutumika nchi nzima.  Hatua hii itakwenda sambamba na kuhakikisha Watendaji kwenye Kata zote 4,066 wanapata vishwambi kuwawezesha kuwahudumia wananchi kupitia mfumo huu wakiwa mahali popote nchini.  

Kwa upande wake Katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI ameziagiza Halmashauri zote ambazo zoezi la majaribio limefanyika na Halmashauri ambazo majaribio yataendelea kufanyika kuhakikisha zinasimamia vyema zoezi  hili kwa kushirikiana na wataalam.

Pia akaagiza kupatiwa taarifa ya utekelezaji kila mwezi. Aidha, Halmashauri zote ambazo zoezi la uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi limefanyika na zenyewe zianze kuwataka wananchi kutumia Anwani za Makazi pindi wanapofika katika Taasisi mbalimbali kupatiwa huduma, Hatua ambayo amesema itatusaidia kutambua vyema watu wanaohudumiwa na hivyo kuongeza ufanisi katika masuala ya ufuatiliaji na tathmini mbalimbali katika huduma.

Awali Waatalam wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari na mawasiliano walionyesha wasilisho lililoonyesha ugumu ambao wananchi walikuwa wakiupata pindi walipohitaji Barua za utamburisho wa mkaazi kwenye ofisi za watendaji ambapo walichelewa kupata huduma husika kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, uhaba wa miundombinu na umbali.

“Barua kwenye ofisi za watendaji ilikuwa kama Donda ndugu lisilotibika kwa wananchi hali iliyowasababishia kukosa huduma za msingi kwa wakati, ndiyo maana serikali imekuja na mfumo wa anwani za makazi ambao ni mwarobaini ….”, amesema

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI