UZALISHAJI WA CHANJO NA DAWA ZA WANYAMA HADI MWAKA 1961 HAKUKUWA NA CHANJO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza leo April 16,2024 jijini Dodoma wakati wa Mkutano na waandshi wa habari kuelezea mafanikio ya sekta ya mifugo na Uvuvi kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano (Picha na Manase Madelemu)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilishirikiana kutokomeza ugonjwa wa Sotoka (Rinderpest) magonjwa yaenezwayo na kupe na udhibiti wa magonjwa yaenezwayo na Mbung'o

Ulega amesema hayo leo April 16 jijini Dodoma wakati wa Mkutano na waandshi wa habari kuelezea mafanikio ya miaka 60 ya Muungano.

"Mbung'o anaeneza ugonjwa wa Nagana kwa Mifugo na Malale kwa binadamu mwaka 1997 kwa mfano Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweza kutokomeza Mbung'o aina ya Glossina austeni na ugonjwa wa Nagana katika kisiwa cha unguja"amesema


Aidha amesema kuwa uzalishaji wa chanjo na dawa za wanyama hadi mwaka 1961hakukuwa na chanjo ya mifugo iliyokuwa ikizalishwa ndani ya nchi, uzalishaji wa chanjo ulianza mwaka 1984 ambapo aina tatu za chanjo za magonjwa ya mifugo zilianza kuzalishwa ambapo ni chanjo ya ugonjwa wa chambavu.

Pia ameongeza kuwa kupitia taasisi ya chanjo Tanzania (TVI) iliyopo kibaha aina ya chanjo za magonjwa ya mifugo zinazozalishwa ndani ya nchi zimefika saba chanjo hizo ni Mdondo kwa kuku,kimeta kwa Ng'ombe,Mbuzi na kondoo,chambavu kwa ng'ombe 


Kuhusu Ujenzi wa miundombinu ya mifugo Ulega amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha shilingi bilioni 51.66 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu katika sekta ya Mifugo na miundombinu iliyoimarishwa ni pamoja na Ujenzi wa miundombinu ya minada ya mifugo ya kisasa 51, Ujenzi wa majosho 746, Ujenzi wa vituo 10 vya kukusanyia Maziwa, Ujenzi wa mabwawa 15,na Ujenzi wa miundombinu Katika vyuo vya mifugo.

Katika hatua nyingine Ulega amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi itahakikisha kuwa sekta ya Mifugo inaendeshwa kibiashara ili kuleta tija kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Vilevile itahakikisha kuwa rasilimali za Uvuvi zinasimamiwa ipasavyo ili kuwa na Uvuvi na ukuzaji viumbe maji endelevu.

(Imeandikwa na Manase Madelemu)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI