UJENZI WA SEKONDARI MPYA 12: FAMILIA MOJA YAJITOLEA KUCHANGIA TSH MILIONI 30

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana vizuri sana na Serikali yetu kwenye miradi ya ujenzi wa sekondari mpya Jimboni mwetu.


Familia ya Mashenene (na rafiki zao) ya Kijiji cha Kiriba tayari imejitayarisha kuchangia takribani Tsh Milioni 30 kwenye ujenzi wa sekondari mpya itakayojengwa kijijini kwao - hongereni sana!


(a) Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu:


(i) Sekondari za Kata/Serikali: 26

(ii) Sekondari za Madhehebu ya Dini: 2


(b) Sekondari mpya 3

Hizi zinazojengwa kwa mchango mkubwa wa Serikali, na Wanavijiji wanachangia nguvukazi


Sekondari hizi zinajengwa Vijijini Butata (Kata ya Bukima), Kasoma (Nyamrandirira) na Kurwaki (Mugango)


(c) Sekondari mpya 3

Hizi zinazojengwa kwa michango ya Wanavijiji, Viongozi wao, na baadhi ya Wazaliwa wa vijiji vyenye miradi ya ujenzi


Vijijini Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), Muhoji (Bugwema) na Kisiwani Rukuba (Etaro)


+Serikali imeanza kuchangia ujenzi wa Muhoji Sekondari

+Sekondari hizi zitafunguliwa Januari 2025


(d) Sekondari mpya 6

Hizi zinaanza kujengwa mwaka huu na Wanavijiji wenyewe wakishirikisha Viongozi wao, na baadhi ya Wazaliwa wa vijijini mwao:


Vijijini Buraga (Kata ya Bukumi), Chitare (Makojo), Kataryo (Tegeruka), Kiriba (Kiriba), Mmahare (Etaro) na Nyambono (Kata ya Nyambono)


+Familia Mashenene na rafiki zao wamejitayarisha kuchangia takribani Tsh Milioni 30 kwenye ujenzi wa sekondari mpya ya kijijini mwao.


+Matayarisho wa ujenzi wa sekondari hizi mpya yanaendelea. Mbunge wa Jimbo ameishapiga Harambee za awali kwa baadhi ya sekondari hizi.


WITO:

Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Musoma Vijijini, wakiwemo Wazaliwa wa Jimbo hili, wanaombwa kuchangia ujenzi wa sekondari mpya kwenye Kata zetu.


Malengo makuu ya ujenzi wa sekondari mpya ndani ya Kata zetu 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 ni:


(i) kutatua tatizo la umbali mrefu unaotembewa na wanafunzi kwenda masomoni


(ii) kutatua tatizo la mirundikano ya wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa. 


Ongezeko la wanafunzi mashuleni, kwa kila mwaka, ni kubwa!


(iii) miaka michache ijayo elimu ya chini kabisa kwa vijana wetu nchini itakuwa Kidato cha Nne (Form IV). Kwa hiyo, sekondari mpya zinahitajika.


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA