ASANTE SAMIA KWA KUTUMWAGIA MONDO MABILIONI - SAMBALA


Diwani wa Kata ya Mondo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma Mh.Said Sambala amemshukuru  Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Kata ya Mondo fedha nyingi za  miradi ya maendeleo hususan katika   ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii katika kata hiyo. 

Ameitaja mradi hiyo kuwa ni pamoja na sekta ya afya, elimu, maji na mingineyo. Hivyo,  Mheshimiwa Sambala amewataka  wananchi wa Kata ya Mondo  kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais  kwa kuhimiza watoto kwenda shuleni  bila kukosa. Aidha, amewataka wazazi kuwapatia watoto wao  mahitaji ya msingi kikiwemo  chakula. Viile bile ameitaja jamii kujenga utamadunk wa kuwa walinzi wa  miundombinu hiyo ili itumike kwa vizazi vingi vijavyo. 
 
" Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Miatatu kwenye Kata yetu ya Mondo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo elimu" alisema Mheshimiwa Sambala na kuongeza " Vile vile ametuongeza Shilingi Milioni Mia Moja kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Waida. Tunajukumu la kuunga mkono juhudi hizi za Mheshimiwa Rais kwa kutimiza wajibu wetu wa malezi bora kwa watoto wetu pamoja na kuwa walinzi wa miundombinu ya miradi hii ili itumiwe na vizazi vingi vijavyo.


Katika kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo ya  utoro Mheshimiwa Sambala  amemshauri Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bwana Thomas Chorray kuitisha kikao haraka ili kujadili  changamoto hizo na kuzitafutia  ufumbuzi.  "Nadhani kuna haja ya Bodi ya Shule tukutane haraka kuzipatia  ufumbuzi changamoto za shule hii ikiwemo changamoto sugu ya  utoro. Utoro haukubaliki katika zama hizi. Kuwepo kwa utoro tafsiri yake ni moja tu kwamba mahala fulani jamii yetu  hatuko sawa."  Kauli hii ameitoa kufuatia takwimu za wahitimu wa mwaka huu  kuonesha karibu nusu yao  yaani  wanafunzi 103 kati yao wavulana 36 na wasichana 67 wameshindwa kuhitimu kwa sababu ya utoro ikilinganishwa na wanafunzi 112  kati yao wavulana 54 na wasichana 68 waliohitimu leo.

Haya yamejiiri Jumamosi Oktoba 12, 2024 alipokuwa anatoa salamu za Serikali wakati wa mahafali ya 27 ya Shule ya Sekondari Mondo iliyoko Kata ya Mondo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoa wa  Dodoma akiwa Mgeni Maalumu. 

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Sambala  amewataka wahitimu wa miaka ya nyuma kuungana katika kutatua changamoto za shule hii. " Mheshimiwa Mgeni Rasmi  mimi ni mmoja wa wahitimu wa shule hii pamoja na wenzangu  Mkuu wa Shule Msaidizi  na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Shule.   Ninaaomba kutumia fursa hii kuwasihi  wenzangu tuliopo ndani ya Kata hii, na maeneo mengine ndani na nje ya mkoa wa Dodoma  kuunganisha nguvu zetu  na  kuanzisha utaratibu maalumu wa kurudisha fadhila kwa shule yetu. Kupitia njia hii ni dhahiri tutapunguza changamoto zinazoikabili shule yetu pendwa" alisema Sambala.

Vile vile Mh. Sambala  ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa Kata ya Mondo na Wilaya ya Chemba kwa ujumla kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ili kupata sifa ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika   Novemba 27 mwaka huu. "Ninawaomba wananchi wa Kata ya Mondo na Wilaya ya Chemba kwa ujumla tuhimizane kujiandikisha kwenye daftari  la wakazi ilitupate sifa ya kushiriki  uchaguzi huu."  

Mgeni Rasmi katika mahafali haya yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi alikuwa Profesa Fadhil Hamza Mgumia kutoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo Profesa Hozen Mayaya. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma Mh.Said Sambala

Mwanafunzi akisoma risala



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

๐— ๐—•๐—ข๐—ช๐—˜ ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ง๐—œ๐—ฆ๐—›๐—” ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—–๐—›๐—”๐——๐—˜๐— ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—”๐—ฅ๐—˜๐—›๐—˜ ๐Ÿฎ๐Ÿฏ.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA