DC SAME AIBUKIA MTAANI KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MAKAZI

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amepita Mtaa kwa Mtaa kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili waweze kuwa na sifa za kushiriki kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa/Kitongoji Novemba 27 mwaka huu 2024.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo DC Kasilda amesisitiza wananchi ambao bado hawajajiandikisha kutumia vyema siku mbili zilizo baki kufika kwenye vituo kujiandikisha kwani Uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ni muhimu kwa ustawi wa Taifa na ndiyo unatoa dira ya Uchaguzi mkuu wa mwakani 2025 wa Rais, Wabunge na Madiwani.


Aidha amesema Wilaya ya Same ina Vitongoji 503 ambapo kila Kitongoji ni Kituo cha kujiandikisha na jambo la muhimu ni mwananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi linalofanyika kwa muda wa siku kumi kuanzia Oktoba 11 hadi 20.


Pia amesisitiza kuwa kitamburisho cha mpiga kura kinachotolewa na tume ni kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao utafanyika mwakani 2025. hivyo kwa Uchaguzi huu ili mwananchi uweze kupiga kura kuchagua viongozi wa Mtaa/Kitongoji chako lazima ujiandikishe kwenye daftari la mkazi.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI