MKURUGENZI MKUU EWURA AWATAKA WAFANYAKAZI KUZINGATIA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza  wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile, amewataka wafanyakazi wa EWURA, kuhudumia wateja wake kwa kuzingatia Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Ameyasema hayo wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma.
“Leo ni siku ambayo tunakumbushana ushirikiano uliopo kati ya watoa huduma na wapokea huduma, kwa upande wetu, sisi tunajielekeza zaidi kwenye kuzingatia utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja( Client Service Charter)”. alisema Dkt. Andilile.
Dkt. Andilile ameongeza na kusema, “EWURA hatuna bidhaa tunayozalisha, hivyo kama mtu anataka kutathmini utendaji wetu wa kazi ataangalia zaidi namna ambavyo tunatoa huduma kwa wateja”
Dkt. Andilile alimalizia kwa kuwataka Wafanyakazi wa EWURA kuboresha utendaji kazi na ushirikiano ili kufikia malengo ya taasisi.
Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa EWURA ni maafikiano kati ya EWURA na wateja wake, ambao ni wadau wakuu katika shughuli za udhibiti. Mkataba umeorodhesha wadau wakuu wa EWURA, huduma zitolewazo pia viwango vya ubora wa utoaji huduma ambavyo wateja wanatarajia.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wafanyakazi wa EWURA na baadhi ya wateja waliofika katika ofisi hizo kwaajili ya kupata huduma mbalimbali.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza  wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma.
BAADHI  ya wateja waliofika katika ofisi ya EWURA wakimsikiliza Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,(hayupo pichani)  wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma.
 
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akiwahudumia baadhi ya wateja waliofika kupata huduma mbalimbali, katika ofisi za EWURA mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma
    
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile, akisalimiana na baadhi ya wateja waliofika katika ofisi ya EWURA mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akiwa katika picha ya moja na baadhi ya Viongozi wa EWURA mara baada ya  kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akiwa katika picha ya moja na baadhi ya wateja  mara baada ya  kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yaliyofanyika leo Oktoba 7,2024  katika ofisi za EWURA Makao Makuu, jijini Dodoma

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA