DK. NCHIMBI 'ASEPA' NA OFISI ZA CHADEMA ITILIMA

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala akizungumza baada ya kutangaza kuondoka Chadema na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi katika mkutano uliofanyika eneeo la Luguru, Itilima Oktoba 8, 2024.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala akielezea sababu za kujitoa Chadema na  kujiunga na CCM
Wanachama wengine wa Chadema wakipokelewa na Dk. Nchimbi.


Sehemu ya umati uliohutubiwa na Dk. Nchimbi katika eneo hilo.


💠 Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima, Katibu na wanachama wao wahamia CCM.


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Ndugu Terry Kilugala, na Katibu wake wa Wilaya ya Itilima, Ndugu Gershom Migasa Mipawa, pamoja na wanachama wao zaidi ya 60, wamehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Luguru, wilayani Itilima.


Ndugu Kilugala, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema mbali na Chadema kuwatumia vibaya viongozi na wanachama wake, kisha kuwaacha ‘watupu’ wakiangaliana wenyewe kwa wenyewe, uongozi wa CCM na utendaji kazi wa serikali yake, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, vyote vimemfanya arudi nyumbani.


“Tulikuwa tunaenda Mwanza siku mbili kwa ubovu wa barabara, leo tunaenda na kurudi. Lazima tuseme ukweli, CCM imefanya kazi, lakini wenzetu wamebakia kusema uongo na kututumia vibaya. Kuna wabunge wa COVID-19, lakini ndani yake wamo wake zao, alafu huku wanatudanganya.”


Balozi Nchimbi, akiwapokea, amesema:


“Hawa ndugu zetu wameona mbali mapema, maana viongozi wakubwa kama Peter Msigwa kaona shida zao, wewe unasubiri nini? Rudini CCM, na nawapongeza wote mliojiunga na CCM, viongozi pamoja na wanachama. Karibuni sana tufanye kazi ya kujenga taifa pamoja.”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA