NDOGO WA MUME WANGU ALIKUWA EX WANGU


 Mdogo wake wa mume wangu alikuwa mpenzi wangu wa zamani kipindi nasoma shahada yangu ya kwanza.


 Kabla ya harusi yangu, nilitaka kumwambia mume wangu, lakini Ex au mpenzi wangu wa zamani ambaye ni mdogo wake alinikatalia kwamba nisimjulishe kwa sababu mume wangu angekatisha harusi yetu mara Moja.


Hivyo, Sikuweza kujieleza kwake kumwambia kuwa nilishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mdogo wake kwa sababu nampenda sana Mume wangu na sikupenda aumizwe na mapito yangu ya zamani. 


Baada ya harusi yetu, ndipo nilipogundua kwamba mpenzi wangu wa zamani alikuwa akiishi na kaka yake au mume wangu. Hivyo basi akaendelea kuishi nasi kwa sababu mume wangu bado hakuweza kupata nyumba inayofaa kwa ajili yake au kumpangishia popote maana ametoka kwenye hekaheka za harusi. 


Kwakweli upendo wa mume wangu kwangu uliongezeka zaidi miezi mitatu baada ya ndoa yetu, hatimaye nikajipata Niko na mimba ya mwezi 1. Lakini mimba hii ikaanza kuleta shida kidogo nikapelekwa hospitali. Nilivyopelekwa hospitali shemeji ndiye alikaa na mimi pale hospitali kwa sababu ya kazi ya mume wangu haikuweza kumruhusu na Kupata muda wa kuja kunifanyia uangalizi hospitali.

Nilikaa wiki moja hospitalinib pale, na tukio hili lilitufunga Kwa kuwa pamoja Mimi na shemeji yangu, kitendo Cha kuwa pamoja hospitalini pale kulianza kunirejesha kumbukumbu za kama tuko kwenye mahusiano kama mwanzo. Lakini nilijitahidi kuua mawazo haya mabaya.


Basi, miezi miwili baadaye, shemeji yangu alipoteza kazi yake, kitu ambacho kilitufanya kuwa pamoja wawili tu pale nyumbani pamoja. 


Japo tulikuwa tunabaki wawili tu baada ya mume wangu kwenda kazini ilinifanya nimwamini na kumheshimu shemeji yangu kwani tulikuwa watulivu sote wawili nami nikawa mtulivu kabisa kama hatujawahi kuwa pamoja.


 Hatimaye nikadhani shemeji yangu alikuwa ameshanikubali kama shemeji yake, lakini kumbe nilikuwa nafanya makosa kumuamini kupiliza. Basi, alasiri moja, nilikwenda ndani kulala na kusahau kufunga mlango wa chumba changu. Shemeji yangu aliingia chumbani kwangu, akanivuta haraka sana na kuanza kufanya tendo na mimi, nilijitahidi kumsumbua na kumsukuma lakini haikusaidia kitu na hapakuwa na usaidizi wowote kwani tunaishi peke yetu.


Baisi Mume alivyorudi kazini sikumwambia mume wangu kwamba nililala na mdogo wake tena Kwa kunilazimisha. Niliwaza je, nitamwambiaje haya yote bila kufichua kuwa niliwahi kuwa na mahusiano na kaka yake hapo awali KABLA hajanipata na kuwa naye kama Mume wangu?.


 Mpaka Hapa Sasa hivi nilivyo Nina kovu moyoni mwangu Hata sijajua litaponaje ambalo naona kama vile shetani ameshaingilia ndoa yangu jamani, naona kama nadhulumiwa na huyu kijana. Wiki nzima hii nimejawa na hasira mnoo. Mume wangu hajui kwanini nimekuwa hivi na hasira hizi yeye anajua tu hii ni Kwa sababu ya ujauzito nilionao. 


 Ninampenda mume wangu sana, na yeye pia ananipenda ila naona Sasa ndoa yangu imeshaanza kuandamwa na shetani...Uh!, nimechoka sana Kwa mkanganyiko huu nidaidieni wandugu.


Enyi ndugu, dada, kaka, mama na baba zangu tafadhali, nifanye nini? Niko kimya naugulia moyoni tu mwenyewe ila leo nimeona nije Hapa kwenu labda ninaweza kupata msaada wa mawazo hata nikapona kabisa".


nikiwa chumbani saa zingine najipata nalia mwenyewe maana Sina pakuanzia..Oh Mungu wangu...Ah!.


Tafadhali, nipo Njia panda jamani, nifanyejeee?."😭


👋👋👋


Makange Avu A.

211201006024000.

06th, October, 2024.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA