RC ANDENGENYE AMEJIANDIKISHA, AHAMASISHA WATU WENGI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Oktoba 17, 2024 amejiandikisha katika Daftari la Mkazi la Mpigakura katika Mtaa wa Shede, kata ya Kigoma katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji kata Kigoma na kutoa wito kwa wakazi mkoani humo kujitokeza  kujiandikisha ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.

Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo, Mhe. Andengenye amesema ni muhimu kwa wakazi kujitokeza na kujiandikisha ili kuchagua viongozi wanaowataka ambao pia watasaidia kusimamia utejelezaji wa Shughuli za Maendekeo zinazotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita mkoani Kigoma 

Amesisitiza kuwa,  uchaguzi wa Viongozi katika ngazi ya kijiji na Mtaa ndicho chanzo na Mzizi wa Demokrasia nchini,  hivyo kutokujiandikisha na kushiriki kupiga kura ni kujinyima haki hiyo muhimu ya kupata kiongozi ambaye atatokana na maamuzi ya wananchi wenyewe.

"Nitoe wito kwa wakazi mkoani hapa kujitokeza ili kupata haki hiyo ya kuchagua kiongozi kuendana na matakwa yao na kuepuka malalamiko ya kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua"  amesema Andengenye.


RC akijiandikisha katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji kata Kigoma.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO