RIDHIWANI AJIANDIKISHA, APONGEZA KASI YA UANDIKISHAJI CHALINZE




-Ashukuru kuongezwa kwa vituo vya uandikishwaji kutatua tatizo la umbali


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amefika kijijini kwao Msoga, Chalinze kujiandikisha ikiwa ni kutimiza takwa la katiba la kujiandikisha ili apate nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. 


Akizungumza baada ya kumaliza kujiandikisha , Mh. Kikwete amepongeza sana utulivu katika kipindi hiki cha uandikishaji.

 “…. Amani ni tunu yetu, na muhimu kujitambulisha nayo kwa vitendo na Watanzania wanathibitisha hili kwa vitendo”, alisema Waziri Kikwete.

 Pamoja na kuwapongeza Watanzania kwa utulivu pia alishukuru Serikali kwa kuamua kuongeza vituo vya kujiandikisha kutokana na wananchi kulalamika kutembea umba mrefu kufuata kituo cha kujiandikisha. Waziri Kikwete alisema, “

…. Naishukuru na kuipongeza Serikali kwa maamuzi ya kutuongezea kituo. Kuna watu wanatoka Chalinze mzee, Chahua walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata kituo cha kujiandikisha.

 Lakini kwa uamuzi huu tunataraji namba itaongezeka na matarajio ya wananchi kupata haki yao ya kupiga kura yapatikana. Nakupongeza msimamizi kwa niaba ya tume na serikali. “


Zoezi hili ambalo lilizinduliwa tarehe 11 na Mh. Rais limekuwa na mafanikio makubwa ambapo hadi sasa halmashauri ya Chalinze imefikia zaidi ya 80 na wanaendelea huku kimkoa, wilaya ya Mkuranga ikiendelea kufanya vizuri katika uandikishaji.


Wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki wamesifu, taratibu zilizoandaliwa na usimamizi na sasa wako tayari kwa zoezi lililombele la kuchagua viongozi wa serikali.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO