TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMISI OKTOBA 17, 2024

Trent Alexander Arnold

Real Madrid wameufanya usajili wa mlinzi wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kuwa kipaumbele. (Athletic – Subscription needed)

Liverpool na Manchester City wanavutiwa na Nicolo Barella wa Inter Milan, 27, lakini kiungo huyo wa kati wa Italia yuko kwenye rada za Real Madrid na Atletico Madrid. (Fichajes – In Spanish)

Arsenal wanafuatilia maendeleo ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Slovenia Benjamin Sesko, 21, huku wakianza kujipanga kwa ajili ya usajili wa dirisha lijalo. (Football London)

Crystal Palace haiko tayari kukaribisha ofa zozote kwa mshambuliaji wa Senegal Ismaila Sarr, 26, mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United wamemuongeza mkufunzi wa Uturuki na mshambuliaji wa zamani wa Italia Vincenzo Montella, 50, kwenye orodha yao ya watu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya mkufunzi wa Uholanzi Erik ten Hag, 54, Old Trafford. (Ajansspor – in Turkish).Vincenzo Montella

Ten Hag atalazimika kuboresha matokeo na kiwango cha mchezo Manchester United ikiwa anataka kusalia katika timu hiyo baada ya mapumziko yajayo ya kimataifa. (Mirror), nje

Manchester United wanapanga wachezaji wa kiungo cha kati watakaochukua nafasi ya kiungo wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, 32, pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Casemiro, 32. (Football Insider).

United pia wako tayari kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 27, ikiwa ataondoka Barcelona msimu ujao. (Fichajes – In Spanish),

Real Madrid wanafikiria kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Josh Acheampong Januari 18, huku Liverpool, Newcastle na Tottenham pia wakimtaka beki huyo wa kulia wa Chelsea. (Independence)


Josha Achiempong

Crystal Palace wanamtafuta David Moyes, 61, kuchukua nafasi ya meneja Oliver Glasner, 50, baada ya kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza. (Caughtoffside)

Uteuzi wa Thomas Tuchel kama meneja wa Uingereza umeongeza matumaini ya Newcastle ya kumsajili mlinzi wa Uingereza na Crystal Palace Marc Guehi, 24, huku Eddie Howe sasa akiwa na uwezekano mkubwa wa kusalia St James' Park. (Givemesport),

Liverpool wako kwenye mazungumzo na Sevilla kuhusu kumnunua mlinzi wa Ufaransa Loic Bade, 24. (Todo Fichajes – In Spanish)

Kiungo wa kati wa Newcastle United Isaac Hayden, 29, amekubali kuiwakilisha Jamaica katika ngazi ya kimataifa, baada ya hapo awali kuichezea Uingereza katika kila kundi la umri kutoka chini ya miaka 16 hadi chini ya miaka 21. (TeamTalks)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO