ZAIDI YA VITUO 80,000 VIMETENGWA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA


 Zaidi ya vituo 80,812 vimetengwa Nchi nzima kwa ajili ya uandikishaji katika daftari la  uchaguzi wa Serikali utakaofanyika Novemba  27, 2024.


Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dodoma Oktoba 10, 2024.

"Kuanzia kesho tarehe 11 Oktoba mpaka tarehe 20 Oktoba,  2024 kutafanyika zoezi la kuandikisha Watanzania wenye sifa kwenye orodha ya wapiga kura kwenye maeneo yao. Zoezi litafanyika katika vituo zaidi ya 80,812 vilivyopo nchi nzima," amesema Makoba.


Kutokana na umuhinu wa uchaguzi huo wa  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewakumbusha Watanzania wote umuhimu wa kushiriki zoezi hilo kwa maendeleo ya taifa.


#Kauli mbiu ya mwaka huu wa uchaguzi ni “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki kwa Uchaguzi”. 


"Zoezi hilo ni muhimu kwani mwananchi atakuwa na sifa ya kupiga kura endapo atakuwa amejiandikisha katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa."


Makoba ametaja sifa za mpiga kura wa uchaguzi huo kuwa ni; lazima awe Raia wa Tanzania, awe na umri wa miaka 18 au zaidi, awe ni mkazi wa eneo la kitongoji au mtaa husika, pia awe na akili timamu.


"Serikali inawasihi wadau wote husika kuendelea kutoa elimu ya uraia ili Watanzania wasichanganye kujiandikisha kwenye orodha ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwani kumekuwa na mkanganyiko kati ya uandikishwaji huu na uandikishwaji na kuboreshwa kwa daftari la kudumu kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025," alimazia kusema Makoba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA