Na Thadei Ole Mushi.
Kuna tetesi kuwa Lisu atapata fursa ya kulihutubia bunge la Umoja wa Ulaya (EU). Lakini kuna tetesi pia kuwa Lisu ataendelea na ziara hiyo na kinachotafutwa Sasa ni connection ya kupata fursa ya kuhutubia bunge la Marekani lakini pia kukutana na Viongozi wa UN. Hoja kubwa ni kuelezea Demokrasia Tanzania na uchaguzi Tanzania ulivyokwenda.
Matokeo ya Ziara hii Kama tetesi hizi zitakuwa za kweli zitapelekea Taifa letu kukutana na vikwazo vya kiuchumi hapa na pale na Hali ya maisha yetu yatakuwa magumu Sana.
Kipindi Cha ukoloni Viongozi wetu wa kiafrika waligawanyika Mara mbili. Kuna kundi lililokuwa likipinga ukoloni kwa vitendo na kundi la Pili waliamua kuungana na wakoloni.
Historia inatuambia kuwa sababu kubwa ya Viongozi wetu kuungana na wakoloni ilikuwa sio fedha bali waliamua kuungana na mkoloni lengo ni kujilinda dhidi ya washindani wao. Mfano kule kwetu Uchagani Mangi Mandara aliamua kuungana na mjerumani kwa lengo la kumshinda Mangi Sina ambaye alikuwa akimsumbua Sana. Inawezekana Lisu naye akaangukia kundi hili la kina Mandara.
Mandara Mpaka leo historia inamhukumu na ni mojawapo ya Mangi asiyeheshimika kabisa Uchagani kutokana na tabia yake hiyo.
Nimejaribu kufuatilia baadhi ya Viongozi wa Upinzani na watu ambao waliwahi Kugombea Urais Africa ni kiongozi gani aliwahi kwenda kuhutubia au kufanya fitna ambayo Lisu anataka kuifanya kwa lengo la nchi yake kuwekewa vikwazo sikuona hata mmoja. List ifuatayo toka jarida la The African Exponent linataja wanasiasa kumi imara kabisa wa Upinzani ambao wametikisa nchi zao lakini taarifa zinatuambia hawakuwahi kwenda kushitaki kwa mabeberu.
1.Bob wine (Uganda) huyu ni Moja ya Mtu anayemsumbua Sana Museven pale Uganda. Aliwahi kupigwa na Polisi Hadi kuvunjika mguu, alitibiwa nje ya nchi na baadaye alirejea nchini kwake na Sasa anagombea urais Uganda. Mwanzoni alionekana Kama anataka kuanza tabia za kuishitaki nchi yake kwa wakoloni wetu wa zamani lakini waliokaribu naye walimshauri akarudi nchini kwake.
2. Julias Sello Malema ( Africa Kusini). Aliwahi kugombana Sana na Zuma na ndiye Mbunge anayeongoza kwa kutolewa nje ya bunge pale Africa Kusini lakini hajawahi kufikiria kutafuta huruma kwa mabeberu au kuishtaki nchi yake. Malenma anaamini matatizo ya Afrika kiuchumi na kisiasa yanaweza kumalizwa na wao wenyewe bila kushirikishwa mkoloni.
3. Diane Rwigara (Rwanda). Mwanamama huyu anatajwa kama mwanamke jasiri Sana. Kitendo Cha kumpinga Kagame si Kitendo kidogo na 2018 alifungwa Ila alitoka baada ya Miezi kadhaa lakini hakuwahi kufikiria kwenda kufanya anachotaka kufanya Lisu.
4. John Mahama (Ghana). Huyu aliwahi kuwa makamu wa Rais Ghana. Mfuatilieni ni Moja ya Viongozi shupavu kabisa wa Ghana. Hajawahi kufikiria kufanya anachotaka kukifanya Lisu.
5. Riek Machar (South Sudan) huyu aliwahi kuwa makamu wa Rais South Sudan. Kwa sasa ndiye muongoza mapambano ya kuondoa Serikali Madarakani pale South Sudan. Hajawahi kwenda kulishitaki Taifa lake popote pale na juzi juzi aliingia makubaliano na Rais Salva Kiir kuwa wamalize mgogoro wa ndani kwenye nchi yao. Huyu hakuwahi kwenda kuhutubia EU wala kumlilia Beberu
6. Maurice Kamto (Cameroon). Huyu alikuwa mwanachama wa International law commission ya UN. Ni mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Cameron iliyopo Madarakani. Mwaka 2018/2019 aliongoza maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi alikamatwa na kufungwa. Pamoja na nafasi yake UN hakuwahi kufikiria kwenda kuhutubia umoja wa mataifa kuishtaki Serikali yake.
7. Martin Fayul (DR-CONGO). Huyu kila mtu anajua kuwa alishinda Urais pale Congo dhid ya Tshisekedi ambaye aliwekwa pandikizi na Serikali iliyopita. Pamoja na kuonekana kuporwa Ushindi wake hajawahi kufikiria kuondoka kwenda kuhutubia popotea kuhusu nchi yake.
8. Raila Omolo Odinga (Kenya). Raila ni mwanasiasa mkongwe Kenya na kila awamu amekuwa akisuguana Sana na Serikali iliyopo Madarakani. Ni kwa bahati mbaya tu waliingia kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe 2007 lakini Ni mojawapo ya Viongozi wanaolipenda Sana Taifa lake la Kenya. Uchaguzi uliopita walizozana Sana Hadi kujiapisha lakini hakuenda kushitaki popote. Leo hii anaingia Ikulu na Kutoka bila shida na wananchi wa Kenya wapo kwenye utulivu mkubwa.
9. Kizza Besigye (Uganda). Kama Kuna kiongozi wa Upinzani amewahi kupigwa na kufungwa Mara nyingi kwenye nchi yake Basi Warren Kizza Besigye Kifefe anaongoza Africa. Mara nyingine hufungiwa ndani ya nyumba yake hakuna Kutoka hata Mwezi lakini hakuwa kuhutubia popote kulisema Taifa lake.
10. Omeleye Sowore (Nigeria). Huyu anamsumbua Sana Buhari pale Nigeria. Mwaka 2019 alikamatwa na kushikiliwa kwa kosa la kutaka kuanzisha fujo. Baada ya kuachiwa hakuwahi kuhutubia popote pale.
Hawa Ni wanasiasa kumi Bora wa Upinzani Africa. Hawa wanaelewa kushitaki Taifa lao kwa Beberu Ni kukaribisha kukaribisha upya ukoloni kwenye nchi yake.
Fact.
Kama Lisu atafanikiwa kwenye mipango yake Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi. Vikwazo hivi havitawaathiri Wanaccm pekee Bali vitamuathiri Hadi asiye na chama aliyepo kule Ikungi Singida.
Ninachokijua familia za Viongozi na yeye Lisu na Familia yake watakuwa watu wa Mwisho kuathirika na vikwazo vutakavyiwekwa hivyo wakati tukiendelea kukenua tujue kuwa athari zozote za Uchumi zitakazolikumba Taifa Basi wa kwanza kuathirika Ni mm na wewe.
Zimbabwe ikiwekewa vikwazo miaka na miaka lakini watoto wa Mugabe walitajwa Kwenye list ya watoto wa Viongozi wanaokula Bata zaidi duniani. Vikwazo vilikuwa vinawahusu wananchi wa Hali ya chini kabisa.
Kwangu Mimi pamoja na misukosuko yote ya kisiasa aliyowahi kupata Mbowe bado hakuwahi kuvuka mstari wa usaliti kwa nchi yake. Ndio maana Mbowe bado kwangu anabaki kuwa Moja wa Viongozi wa Upinzani wenye maono na Busara kubwa Sana.
Ninaamini Bado pande zote zinazokinzana zina fursa ya kujadiliana. Ninaamini bado Lisu akishauriwa na wazalendo wa nchi hii anaweza kupata fursa ya kufikiri upya.
Tatizo ninaloliona tumemwachia Lisu ashauriwe na mabeberu. Kitendo Cha kuwaachia mabalozi wa mataifa ya magharibi wamshauri tulikosea Sana Kama taifa. Hakuna mahali mataifa ya Magharibi yanaweza kumpenda Lisu na sisi watanzania kuliko sisi wenyewe.
Anyway ngoja tuone lakin njia anayoitumia Lisu kujijenga kisiasa Ina miba mingi Sana na inaweza kuja kumhukumu baadaye.
Ole Mushi.
0712702602
Comments