CCM INAHITAJI SUBIRA - CPA MAKALLA

 Na Mwandishi Wetu


KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makalla ametoa wito kwa waliyokuwa wagombea wa chama hicho katika nafasi za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao majina yao hayakupitishwa pamoja na kwamba walishinda kura za maoni, kuwa na Subira..

Makalla ameyazungumza hayo  jijini Dar es Salaam katika mkutano wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni.


Pia amewapongeza baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa na bado wanaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama hicho, akijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba kuna kipindi aligombea na kushinda kwa kishindo lakini jina lake halikurudi.

“Tunawatakia kila la kheri waliokosa uvumilivu, wako ambao hata uteuzi haujafanyika wakahamia mtaa wa pili siku ya tatu wakageuza tena CCM, niwape salamu hao waliowaokoteza tumewaazima tuu wagombea watarudi Chama cha Mapinduzi,” alisema na kuongeza:

“Kuna wengine hata vikao hatujakaa niliona wanakaribishwa siku mbili jamaa akarudisha kadi akarudi CCM, hivyo niwaombe kuweni watulivu tuna uchaguzi mwakani,” amesema Makalla.

Aidha, amesema uchaguzi wa awamu hii hauna kupita bila kupingwa, hivyo waombea na wanachama wa chama hicho wasibweteke, akisisitiza kwamba wako imara na hawatalala.

Amesisitiza kwamba watahakikisha hata pale watakapokuwa wako pekeyao watafanya kampeni na kuhakikisha wagombea wao wanapata kura za ndio.

“Anaesubiri kumuangusha mgombea wa CCM kwa kura za hapana ni sawa na mtu anaesubiri ndege bandarini badala ya ‘Airport’ wanaccm nchini kote tuchangamke hakuna neno ‘Mama’ tukamilishe hiyo kazi, mahali patakapothibitika tuko sisi tutafanya kampeni ya kutosha wagombea wetu wote wapite kwa kishindo,” amesema Makalla.

Katika picha mbalimbali.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni katika Ukumbi wa Kiramuu Hall, Novemba 04, 2024. (Picha na Fahadi Siraji)





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE