Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana vizuri na Serikali yetu kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zao za kata.
Malengo makuu ya ujenzi huo ni:
(i) kuongeza na kuboresha ufundishaji, uelewa na ufaulu mzuri kwenye mitihani ya masomo ya sayansi
(ii) kuongeza idadi ya "high schools" za masomo ya sayansi Jimboni mwetu
Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu (Kata 21):
(i) Sekondari za Kata/Serikali: 26
(ii) Sekondari za Binafsi: 2
(iii) Sekondari mpya zinazojengwa: 10
Idadi ya high schools Jimboni mwetu:
(i) Kasoma High School: masomo ya "arts"
(ii) Suguti High School: masomo ya sayansi kuanzia mwakani, 2025
(iii) Mugango High School: masomo ya sayansi kuanzia mwakani, 2025
Sekondari zinazojenga kwa kasi miundombinu ya uanzishwaji wa "high schools" za masomo ya sayansi:
(iv) Mtiro Sekondari (v) Makojo Sekondari
(vi) Kiriba Sekondari (vii) Etaro Sekondari
Ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya kuanzishwa kwa Mtiro High School:
Mtiro Sekondari ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 654.
Sekondari hii ni ya Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne, ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera.
Miundombinu inayojengwa kukidhi viwango vya kuanzishwa "high school" ya masomo ya sayansi ni:
(i) Maabara 3 za masomo ya Physics, Chemistry na Biology
Michango ya thamani ya Shilingi milioni 31 (Tsh 31m) - Wachangiaji: Wanakijiji, Mbunge wa Jimbo, Mfuko wa Jimbo na Halmashauri yetu (Musoma DC)
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alipiga Harambee mbili (2) za kuanza ujenzi wa maabara hizo.
(ii) Bweni la Wanafunzi
Mchango wa Shilingi milioni 131.4 (Tsh 131.4m) - Mchangiaji: Serikali Kuu
(iii) Vyumba vipya 4 vya Madarasa
Mchango wa Shilingi milioni 100 (Tsh 100m) - Mchangiaji: Serikali Kuu
(iv) Vyoo vipya
Mchango: Shilingi milioni 24.9 (Tsh 24.9m) - Mchangiaji: Serikali Kuu
(v) Maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria: yapo
(vi) Umeme wa REA/TANESCO: upo
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
(i) Maboma ya maabara ya masomo ya sayansi yanayojengwa Mtiro Sekondari
(ii) Vyumba vipya vya Madarasa vinavyojengwa Mtiro Sekondari
SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wote wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye sekondari zao za Kata, na kuongeza idadi ya "high schools", hasa za masomo ya sayansi Jimboni mwetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Comments