Na Angela Sebastian; Bukoba 

MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera.


Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza. 



Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono.


ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja hilo kuchoka kwasababu limejengwa muda mrefu ambalo liko, katika barabara kuu inayounganisha kata zote za Halmashauri ya Bukoba,Misenyi na Karagwe katika kusafiri kutafuta huduma muhimu za wananchi na kusafurisha mazao na bidhaa nyingine.


Jingine ni Chanyabasa ambapo wananchi hutumia kivuko kuvuka toka kata zaidi ya nane kuja hospitali ya Wilaya ya Bukoba Vijijini na wengime wanaovuka kwenda Bukoba mjini kwa shughuli za kujiingizia kipato hari inayosababisha watumie muda mrefu wakisubiri kivuko kwasababu kinavusha watu wachache na mizigo kidogo.



Amesema ujenzi huo unaotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia hivi sasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 kutokana na maagizo ya Serikali hawamu ya sita.


 Ametaja daraja jingine ambalo limeingizwa kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa na fedha yake italetwa wakati wowote kuwa ni Kyetema, linaunganisha barabara kuu kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine kuingia Bukoba na nchi jirani ya Uganda.


"Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Bukoba vijijini tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa kwetu ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yetu mfano madaraja mawili ya Karebe na Chanyabasa ambayo ni lango la mkoa huu ametoa zaid ya shl.bil 19 na mradi mkubwa wa maji Kemondo ambao umekamilika na wananchi wanatarajia kipata maji mwezi mmoja ujao umegharimu shl bl.16"alieleza Rweikiza.


"Mwaka 2019 ilinyesha mvua kubwa na kusababisha daraja la Karebe kutopitika na kuwalazimu wananchi wa kata 18 kuanza kutumia kivuko kidogo cha Chanyabasa ambacho hata hivyo hakikuwa na uwezo wa kuhudumia magari makubwa, baada ya hali hiyo kujitokeza ndipo nilimuomba Naibu waziri wa Ujenzi wakati huo Elias Kwandikwa(Marehemu)afike katika kivuko hicho alifika na kujionea hali halisi ambapo nilitoa maombi kujengwa daraja badala ya kivuko kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi"


Amesema Naibu waziri huyo alikubali na kumuahidi kuwa maombi hayo anakwenda kuyaweka kwenye mpango wa serikali kwa ajili ya kutenga bajeti ya kujenga daraja eneo hilo pia iliwekwa kwenye Ilani ya ChamaChaMapinduzi (CCM).


Naye askofu wa kanisa la kiinjiri la kirutheri dayosisi ya kaskazini magaribi (KKT DKMG) Abedinego Keshomshahara amesema kuwa Serikali ya hawamu ya sita inafanya maendeleo makubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi pia mbunge Rweikiza amekuwa kiungo kizuri kati ya wananchi,Serikali na viongozi wa dini zote.



Kwa upande wa katibu mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM),katibu mkuu kiongozi mstaafu,balozi na mbunge Dk.Bashir Alli amesema ni vizuri watu kutengeneza hadithi zitakazo wavutia wasomaji na wasikilizaji.



 "Tunapo kuwa madarakani kustaafu na baada ya kufa hadithi zetu ziwe nzuri kwa watu kwani maombi ya miradi hiyo ililetwa kwenye chama wakati wa Serikali ya hawamu ya tano na mbunge Rweikiza ambapo tuliingiza kwenye Ilani ila kutokana na maono mema ya Rais Dk. Samia ameamua kutoa fedha nyingi ili ikajengwe na kunufaisha wananchi hiyo ni hadithi nzuri itakayoandikwa milele na kuacha alama"ameeleza Dk Bashir.





















Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI