BUSARA KUTOKA KWA BABA TAJIRI.

Kutoka kwenye kitabu "Rich DAD Poor DAD"

cha Robert Kiyosaki

1. Usifanye kazi kwa ajili ya kutengeneza pesa (Don’t work for money):

Watu matajiri huwa hawafanyii kazi pesa. Kama unaifanyia pesa kazi akili yako itaanza kufanya kazi kama akili ya mwajiriwa. Kama ukianza kufikiri tofauti kama mtu tajiri, utaona mambo kwa namna ya tofauti. Matajiri hufanyia kazi upande wa mali zao, kila sumni kwenye mali zao ni mfanyakazi anayechapa kazi kwa bidii.

2. Usitawaliwe na hisia zako (Don’t be controlled by emotions):

Baadhi ya maisha ya watu yametawaliwa na hisia mbili za hofu na tamaa. Hofu huwafungia watu kwenye mtego wa kuchapa kazi kwa bidii, kutengeneza pesa, kuchapa kazi na kutengeneza pesa na kudhani kuwa kutapunguza hofu zao. Pili, wengi wetu tuna tamaa ya kutajirika haraka. Ndio, wapo watu ambao hutajirika haraka,  lakini wengi wao hawana elimu ya fedha. Hivyo, jielimishe juu ya fedha na usijawe na tamaa. 

3. Nunua Mali (Acquire assets):

Usinunue madeni kwenye safari yako ya kuwa huru kifedha. Watu hununua madeni wakidhani kuwa wamenunua mali. Watu wengi hununua starehe kwanza, kama vile magari makubwa, pikipiki kubwa au kujenga majumba makubwa ya kuishi. Lakini matajiri hununua mali na mali zao hulipia starehe zao. Matajiri hununua majumba na kuyapangisha kisha hutumia kodi wanazokusanya kulipia starehe na vitu vya kifahari. Watu maskini na wachini hununua starehe kwanza na matajiri huchelewa kununua starehe.  

4. Kumbuka Hii Kanunni (Remember the KISS principle):

Fanya mambo kiwepesi na kijinga(KISS stands for keeping it simple, and stupid). Usijichoshe na mambo mengi unapoanza safari yako ya kujiweka huru kiuchumi. Mambo ni mepesi na yafanye kiwepesi. Jambo la kukumbuka ni kuwa mali huweka pesa mfukoni na madeni hutoa pesa mfukoni. Mara zote nunua mali. 

5. Tambua tofauti iliyopo kati ya mali na madeni (Know the difference between assets and liabilities):

Mali ni kitu chochote kinachotia pesa mfukoni mwako, kama vile hisa, amana, majengo na mashamba, vipande, nyumba za kukodosha, nk. Madeni ni chochote kinachotoa pesa mfukoni, kama vile nyumba yako ya kuishi, gari lako, mkopo wako, nk. Watu hufikiri kuwa nyumba zao ndio mali kubwa kwao lakini kiukweli sio. Nyumba ni mali pale ambapo unakusanya kodi, lakini unapoishi ndani yake inakuwa deni.    

6. Usiwe mjinga kifedha (Don’t be a financial illiterate):

Mtu anaweza kuwa na elimu kubwa hadi kuwa na weledi wa juu lakini bado akawa mjinga kifedha. Elimu ya kifedha ni muhimu sana kwa mtu yeyote. Shule zetu na elimu tuliyoisoma haikusisitiza elimu ya fedha. Matatizo mengi yanatokana na ukosefu wa elimu ya kifedha. Anza kujijengea maarifa ya kifedha na nakushauri usome kitabu cha "Rich Dad,Poor Dad"

7. Ongeza Ukwasi Wako (Increase your Wealth):

Ukwasi unatafsiriwa kama uwezo wa mtu wa kuweza kuishi kwa muda fulani kama atakaa bila kufanya kazi. Embu jiulize utaweza kuishi kwa kipindi kirefu kiasi gani bila kufanya kazi? 

8. Jihusishe na Mambo Yako Pekee (Mind your own business):

Kama una ajira, endelea kufanya kazi na uanzishe biashara yako na kuifanyia kazi. Tumia muda unaoutumia kwenye simu janja yako, sherehe, au shughuli nyingine yeyote kujenga biashara yako. Usiache ajira yako hadi pale unapokuwa umejenga biashara yako. Usimfanyie mtu mwingine kazi maisha yako yote. Anzisha biashara yako na uikuze. 

9. Ijenge Akili Yako (Train your mind):

Mali yako kuu ni akili yako. Watu wengi hutazama fursa na macho yao, lakini ukiifunza akili yako, utaweza kuziona fursa kupitia akili yako. Kama ukiijenga akili yako vyema, utaweza kutengeneza ukwasi mkubwa. 

10. Jenga Ujuzi (Learn technical skills):

Uwezo wako wa kifedha utaongezeka kwa kujifunza ujuzi zifuatazo: 

Uhasibu (Accounting): Unatafsiriwa kama uwezo wa kusoma na kutafsiri mahesabu. Kama unataka kujenga himaya yako, tambua kuwa ujuzi huu ni wa msingi. Kwa kujifunza ujuzi huu, utaweza kuelewa nguvu na udhaifu wa biashara yako. 

Maarifa ya Uwekezaji (Investing): Ni sayansi ya kutengeneza pesa.  

Ujuzi wa kusoma na kuyaelewa masoko (Understanding markets): Sayanzi ya kuweza kujua  mahitaji ya soko na upatikanaji wa malighafi (It is the science of supply and demand).

Kuzifahamu Sheria(The Law): Mtu anayetambua maarifa ya sheria za kodi na makampuni anaweza kutajirika kiwepesi zaidi. 

11. Tafuta fursa Ambazo Wengine wote wamezimisi (Find opportunities that everyone else missed):

"Fursa kubwa huwa hazionekani kwa macho. Huonekana kiakili zaidi."

Unaweza kuona fursa nyingi kiakili kuliko zile amabazo watu hushindwa kuziona kwa macho. Sio sayansi ngumu bali unahitajika kuifunza akili yako.  

12. Jifunze Kutawala Hatari(Learn to manage risk):

Kuwekeza sio jambo hatari, bali kutojua jinsi ya kuwekeza ndio jambo hatari. Kama unataka kupunguza hatari, basi ongeza maarifa yako. Maarifa haya hayawezi kuongezeka kwa kwenda chuoni, yatakuja kwa kusoma vitabu ama kukaa na watu wanaojua uwekezaji. 

13. Jifunze Utawala (Learn management):

Maarifa muhimu ya utawala ni:

Utawala wa mzunguko wa pesa,

Utawala wa mifumo

Utawala wa watu

Uwezo wa kuuza na kufanya masoko

14. Tawala Hofu (Manage fear):

"Kufeli huwachochea washindi. Kufeli hupelekea waliofeli kuacha."  

Kila mtu ana hofu ya kupoteza pesa. 

Asante kwa kusoma na kushea πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏBUSARA KUTOKA KWA BABA TAJIRI.

Kutoka kwenye kitabu "Rich DAD Poor DAD"

cha Robert Kiyosaki

1. Usifanye kazi kwaajili ya kutengeneza pesa (Don’t work for money):

Watu matajiri huwa hawafanyii kazi pesa. Kama unaifanyia pesa kazi akili yako itaanza kufanya kazi kama akili ya mwajiriwa. Kama ukianza kufikiri tofauti kama mtu tajiri, utaona mambo kwa namna ya tofauti. Matajiri hufanyia kazi upande wa mali zao, kila sumni kwenye mali zao ni mfanyakazi anayechapa kazi kwa bidii.

2. Usitawaliwe na hisia zako (Don’t be controlled by emotions):

Baadhi ya maisha ya watu yametawaliwa na hisia mbili za hofu na tamaa. Hofu huwafungia watu kwenye mtego wa kuchapa kazi kwa bidii, kutengeneza pesa, kuchapa kazi na kutengeneza pesa na kudhani kuwa kutapunguza hofu zao. Pili, wengi wetu tuna tamaa ya kutajirika haraka. Ndio, wapo watu ambao hutajirika haraka, lakini wengi wao hawana elimu ya fedha. Hivyo, jielimishe juu ya fedha na usijawe na tamaa. 

3. Nunua Mali (Acquire assets):

Usinunue madeni kwenye safari yako ya kuwa huru kifedha. Watu hununua madeni wakidhani kuwa wamenunua mali. Watu wengi hununua starehe kwanza, kama vile magari makubwa, pikipiki kubwa au kujenga majumba makubwa ya kuishi. Lakini matajiri hununua mali na mali zao hulipia starehe zao. Matajiri hununua majumba na kuyapangisha kisha hutumia kodi wanazokusanya kulipia starehe na vitu vya kifahari. Watu maskini na wachini hununua starehe kwanza na matajiri huchelewa kununua starehe.  

4. Kumnuka Hii Kanunni (Remember the KISS principle):

Fanya mambo kiwepesi na kijinga(KISS stands for keeping it simple, and stupid). Usijichoshe na mambo mengi unapoanza safari yako ya kujiweka huru kiuchumi. Mambo ni mepesi na yafanye kiwepesi. Jambo la kukumbuka ni kuwa mali huweka pesa mfukoni na madeni hutoa pesa mfukoni. Mara zote nunua mali. 

5. Tambua tofauti iliyopo kati ya mali na madeni (Know the difference between assets and liabilities):

Mali ni kitu chochote kinachotia pesa mfukoni mwako, kama vile hisa, amana, majengo na mashamba, vipande, nyumba za kukodosha, nk. Madeni ni chochote kinachotoa pesa mfukoni, kama vile nyumba yako ya kuishi, gari lako, mkopo wako, nk. Watu hufikiri kuwa nyumba zao ndio mali kubwa kwao lakini kiukweli sio. Nyumba ni mali pale ambapo unakusanya kodi, lakini unapoishi ndani yake inakuwa deni.    

6. Usiwe mjinga kifedha (Don’t be a financial illiterate):

Mtu anaweza kuwa na elimu kubwa hadi kuwa na weledi wa juu lakini bado akawa mjinga kifedha. Elimu ya kifedha ni muhimu sana kwa mtu yeyote. Shule zetu na elimu tuliyoisoma haikusisitiza elimu ya fedha. Matatizo mengi yanatokana na ukosefu wa elimu ya kifedha. Anza kujijengea maarifa ya kifedha na nakushauri usome kitabu cha "Rich Dad,Poor Dad"

7. Ongeza Ukwasi Wako (Increase your Wealth):

Ukwasi unatafsiriwa kama uwezo wa mtu wa kuweza kuishi kwa muda fulani kama atakaa bila kufanya kazi. Embu jiulize utaweza kuishi kwa kipindi kirefu kiasi gani bila kufanya kazi? 

8. Jihusishe na Mambo Yako Pekee (Mind your own business):

Kama una ajira, endelea kufanya kazi na uanzishe biashara yako na kuifanyia kazi. Tumia muda unaoutumia kwenye simu janja yako, sherehe, au shughuli nyingine yeyote kujenga biashara yako. Usiache ajira yako hadi pale unapokuwa umejenga biashara yako. Usimfanyie mtu mwingine kazi maisha yako yote. Anzisha biashara yako na uikuze. 

9. Ijenge Akili Yako (Train your mind):

Mali yako kuu ni akili yako. Watu wengi hutazama fursa na macho yao, lakini ukiifunza akili yako, utaweza kuziona fursa kupitia akili yako. Kama ukiijenga akili yako vyema, utaweza kutengeneza ukwasi mkubwa. 

10. Jenga Ujuzi(Learn technical skills):

Uwezo wako wa kifedha utaongezeka kwa kujifunza ujuzi zifuatazo: 

Uhasibu(Accounting): Unatafsiriwa kama uwezo wa kusoma na kutafsiri mahesabu. Kama unataka kujenga himaya yako, tambua kuwa ujuzi huu ni wa msingi. Kwa kujifunza ujuzi huu, utaweza kuelewa nguvu na udhaifu wa biashara yako. 

Maarifa ya Uwekezaji(Investing): Ni sayansi ya kutengeneza pesa.  

Ujuzi wa kusoma na kuyaelewa masoko (Understanding markets): Sayanzi ya kuweza kujua mahitaji ya soko na upatikanaji wa malighafi (It is the science of supply and demand).

Kuzifahamu Sheria(The Law): Mtu anayetambua maarifa ya sheria za kodi na makampuni anaweza kutajirika kiwepesi zaidi. 

11. Tafuta fursa Ambazo Wengine wote wamezimisi (Find opportunities that everyone else missed):

"Fursa kubwa huwa hazionekani kwa macho. Huonekana kiakili zaidi."

Unaweza kuona fursa nyingi kiakili kuliko zile amabazo watu hushindwa kuziona kwa macho. Sio sayansi ngumu bali unahitajika kuifunza akili yako.  

12. Jifunze Kutawala Hatari(Learn to manage risk):

Kuwekeza sio jambo hatari, bali kutojua jinsi ya kuwekeza ndio jambo hatari. Kama unataka kupunguza hatari, basi ongeza maarifa yako. Maarifa haya hayawezi kuongezeka kwa kwenda chuoni, yatakuja kwa kusoma vitabu ama kukaa na watu wanaojua uwekezaji. 

13. Jifunze Utawala (Learn management):

Maarifa muhimu ya utawala ni:

Utawala wa mzunguko wa pesa,

Utawala wa mifumo

Utawala wa watu

Uwezo wa kuuza na kufanya masoko

14. Tawala Hofu (Manage fear):

"Kufeli huwachochea washindi. Kufeli hupelekea waliofeli kuacha."  

Kila mtu ana hofu ya kupoteza pesa. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI