MTANZANIA Mkali wa Mbio Ndefu, Alphonce Felix Simbu, ameshika nafasi ya nne akikimbia kwa muda wa saa 2, dakika 4 na sekunde 38 (2:04:38 PB), kwenye mbio za Valencia Marathon 2024, zilizofanyika mapema leo huko Valencia nchini Hispania.
Mwanariadha wa Ethiopia, Dress Geleta alishika nafasi ya pili baada ya kutumia saa 2 dakika mbili na sekunde 38 (2:02:38), huku Mkenya Sebastian Sawe akiibuka kinara kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 2 na sekunde tano (2:02:05) na kutwaa medali ya Dhahabu.
Matokeo hayo, yanakuja wiki moja tu tangu Simbu na Magdalena Crispine Shauri walishinda Medali za Dhahabu kwa muda wa 2:17:19 na 2:36.29 kwenye Mashindano ya Majeshi Afrika (AMGA 2024) yaliyofanyika huko Abuja , Nigeria.
Comments