π— π—žπ—”π—‘π——π—”π—₯π—”π—¦π—œ 𝗖𝗝π—₯π—˜ π—”π—§π—”π—žπ—œπ—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—žπ—”π—•π—œπ——π—›π—œ π—π—˜π—‘π—šπ—’ π—Ÿπ—” π—ͺπ—œπ—­π—”π—₯𝗔 𝗬𝗔 π—˜π—Ÿπ—œπ— π—¨

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya China ya CRJE inayotekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kukamilisha miundombinu yote ikiwemo ya TEHAMA kuhakikisha inawezesha utoaji wa huduma kikamilifu.

Prof. Nombo ametoa agizo hilo Januari 08, 2025 wakati akikagua jengo hilo ambapo amesisitiza kuwa
makabidhiano ya jengo hilo yatafanyika Januari 9, 2025, na kwamba ni muhimu kuzingatia maelekezo yote.

Prof. Nombo pia amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu Ufundi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Fredrick Salukele kutumia timu yake ya wahandisi kufanya ukaguzi 𝘱𝘳𝘦-π˜ͺ𝘯𝘴𝘱𝘦𝘀𝘡π˜ͺ𝘰𝘯 kwa niaba ya watumiaji wa jengo hilo kabla ya kukabidhiwa jengo.

Katibu Mkuu huyo amemsisitiza Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanakagua kikamilifu vifaa vyote.

Profesa Nombo akitwa na viongozi wengine wakikagua maendeleo ya  ujenzi huo.

Prof. Nombo akizungumza alipotembelea jengo hilo.Matukio mbalimbali ya Prof. Nombo alipotembeleo kuona maendeleo ya ujenzi wa jango hilo.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

DK. KIKWETE AZINDUA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI, APONGEZA MAENDELEO ZANZIBAR

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN