KAMATI YA MFUKO WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI YAGAWA VIFAA VYA UJENZI*



Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameitisha Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kwa lengo la kugawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo.


*Waliohudhuria Kikao hicho:*

(i) Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo

(ii) Sekretariati ya Mfuko wa Jimbo

(iii) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji

 vilivyotuma maombi

(iv) Wakuu wa Sekondari zilizotuma maombi


*Fedha za Mfuko wa Jimbo:*

Tsh 75,796,000 (Tsh 75.796m)


*Vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa:*

(i) Saruji Mifuko: 1,970

(ii) Mabati ya rangi: 322

(iii) Nondo, 8mm: 430


*Orodha ya Sekondari zilizogawiwa vifaa vya ujenzi:*


(i) Sekondari zinazojitayarisha kufunguliwa -

Muhoji, Nyasaungu na Rukuba (Kisiwa)


(ii) Sekondari zinazokamilisha ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi -

Mtiro, Makojo, Nyambono, Bwai, Mkirira na Etaro


(iii) Sekondari zinazoanza ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi - Bukwaya na Nyanja


(iv) Sekondari mpya zinazoanza ujenzi -

Chitare (Kata ya Makojo), Mwigombe (Kata ya Kiriba), Mmahare (Kata ya Etaro), Musanja (Kata ya Musanja), Kataryo (Kata ya Tegeruka) na Nyabakangara (Kata ya Nyambono)


*Vifaa vya ujenzi vilivyogawiwa:*

Kiambatanisho kilichowekwa hapa kinajieleza ipasavyo.


*Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:*

Washiriki wa Kikao cha Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini. Kikao kimefanyika leo, Kijijini Suguti, Makao Makuu ya Halmashauri yetu (Musoma DC)


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 


P. O. Box 6

Musoma 


Tarehe:

Jumanne, 7 Jan 2025

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

DK. KIKWETE AZINDUA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI, APONGEZA MAENDELEO ZANZIBAR

KOCHA WA MAMELODI ASIMAMISHWA KWA KUWAPIGA CHABO WACHEZAJI WAKE WA KIKE