Yanga SC imeendelea kuonyesha ubabe wake kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa Mashujaa FC mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Ushindi huu unaiweka kileleni mwa msimamo wa ligi kwa pointi 55.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Duke Abuya (33’), Prince Dube (49’), Khalid Aucho (55’), Clatous Chama (74’, 83’). Ushindi huu unaifanya Yanga kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza ugenini msimu huu, ikiwa imeshinda mechi 9 kati ya 10 na kutoka sare moja.
Mashujaa, ambao kabla ya mechi hii walikuwa wameruhusu mabao matatu pekee katika mechi 10 za nyumbani, leo wamevunjwa rekodi yao kwa kuruhusu mabao mengi zaidi kuliko walivyowahi kuruhusu kwenye mechi zote za awali nyumbani. Kichapo hiki kinawaacha na pointi 23, wakiendelea kuwa hatarini kushuka daraja.
FOLLOW US
Comments