EAST AFRICA NA DP WORLD ZATAJWA MAFAINIKIO YA TPA MIAKA 4 YA DKT SAMIA.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bwana Plasduce Mbossa amesema kuwa Shehena ya Makasha iliyohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7 kwa mwaka,kutoka Makasha 816,368 mwaka 2021/2022 hadi Makasha 998,872 mwaka wa fedha 2023/2024.


Ameswma kuwa ngezeko hilo limetokana na maboresho ya uendeshaji wa vitengo vya makasha vya Bandari hiyo kwa kuviweka chini ya uendeshaji wa Sekta binafsi ya Kampuni DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited zilizowekeza kwa kufunga mitambo ya kisasa.


Mbossa ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Februari 24,2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari akielezea mafanikio ya TPA kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt Samia. 


Na kuongeza kuwa katika kipindi hiki shehena iliyohudumiwa na Mamlaka hii imekuwa ikiongezeka  kwa wastani wa asilimia 15.23 kwa mwaka kutoka tani milioni 20.78 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 27.55 Mwaka wa Fedha 2023/2024.


Na kusema kuwa  shehena ya Makasha yenyewe imeongezeka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka kutoka makasha 823,404 mwaka 2021/22 hadi Makasha 1,050,486 mwaka 2023/24.


"Ndugu Wanahabari Jumla ya shehena ya Makasha (Containers) iliyohudumiwa imeongezeka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 823,404 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 1,050,486 Mwaka wa Fedha 2023/2024. Aidha, jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM imeongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 816,368 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 998,872 Mwaka wa Fedha 2023/2024".



"Ongezeko la makasha katika Bandari ya Dar es Salaam limetokana na maboresho ya uendeshaji wa vitengo vya makasha vya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuviweka chini ya uendeshaji wa Sekta Binafsi wa Kampuni ya DP World Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) ambazo zimewekeza kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kuhudumia shehena pamoja na mifumo ya kisasa ya TEHAMA ya uingizaji na uondoshaji wa makasha bandarini".



"Katika kipindi hiki jumla ya shehena iliyohudumiwa na TPA imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 15.23 kwa mwaka kutoka tani milioni 20.78 Mwaka wa Fedha   2021/22 hadi tani milioni 27.55 Mwaka wa Fedha 2023/2024.


 Aidha, jumla ya shehena iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM iliongezeka kwa wastani wa asilimia 13.38 kwa mwaka kutoka tani milioni 18.67 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 23.98 Mwaka wa Fedha 2023/2024.


 Ongezeko la shehena limetokea baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kukamilisha miradi mbalimbali ya ujenzi na maboresho ya miundombinu ya Bandari nchini ikiwa ni pamoja na kukamilisha mradi wa maboresho na uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam (Dar es Salaam Maritime Gateway Project – DMGP) ambao umewezesha kuanza kuja kwa meli kubwa zilizokuwa zinashindwa kuja katika Bandari ya Dar es Salaam kabla ya maboresho na uendelezaji huo kufanyika".


Aidha Mbossa amesema pamoja na utendaji kazi mzuri wa Mamlaka hii lakini bado sekta ndogo ya bandari imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa gati zinazoweza kukidhi idadi na ukubwa wa Meli,uchakavu wa miundombinu ya bandari, Ukosefu wa rasilimali fedha, ukosefu wa Meli na vyombo vya kisasa vya usafiri wa Maji na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.


"Ndugu Waandishi wa habari Pamoja na utendaji kazi mzuri ulioainishwa hapo juu bado sekta ndogo ya bandari inakabiliwa na changamoto kuu zifuatazo:

Uchache wa gati zinazoweza kukidhi ongezeko la idadi na ukubwa wa meli.Uchakavu wa miundombinu ya bandari na isiyokidhi mahitaji ya meli za kisasa.Ufinyu wa maeneo ya kuhudumia na kuhifadhi shehena.

Ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu.Miundombinu wezeshi (barabara na reli) isiyokidhi mahitaji ya ukuaji wa shehena.

Meli zingine kuamua kwenda bandari shindani kutokana na changamoto za muda wa huduma na ufanisi.Ukosefu wa meli na vyombo vya kisasa vya usafiri wa maji.Mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri operesheni katika bandari zetu za maziwa".



Aidha amesema Serikali kupitia TPA imendelea kufanya jitihada ili kuimarisha uwezo na ufanisi wa utoaji wa huduma za kibandari kwa kujenga Bandari mpya zenye vifaa vya kisasa ikiwemo gati mpya mbili zenye urefu mita 500 na gati jipya la kuhudumia mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam. 



"Serikali kupitia TPA imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ilikuhakikisha uwezo na ufanisi wa utoaji huduma za kibandari nchini unaimarika zaidi kwa kujenga Bandari mpya zenye vifaa vya kisasa ikiwemo gati mpya mbili zenye urefu mita 500 na gati jipya la kuudumia mafuta katika Bandari ya Dar es salaam, Uendelezwaji wa eneo lililokuwa la EPZA ili liweze kutumika kuhudumia shehena na Uendelezaji wa Bandari ya Kigoma, Tanga, Bandari Kavu na maeneo mengine nchini kulingana na uhitaji wa soko".


Sambamba na hayo hakiacha kugusia suala la mchango wa Mapato kwa Nchi kupitia Mamlaka hii ambapo amesema Bandari ya Dar es Salaam inahudumia zaidi ya asilimia 95 ya shehena zote zinazopitia katika Bandari za Tanzania kwenda nchi jirani na hivyo kuchangia kiasi kikubwa katika makusanyo ya kodi kwani Dar es Salaam kuna Taasisi za Umma zaidi ya 30 zinazotoa huduma mbalimbali za bandari, mfano wa mapato yaliyokusanywa na TPA tu kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Juni 2024 yamefikia Shilingi Trilioni 1.4  na kwa mujibu wa taarifa ya TRA mapato yatokanayo na ushuru wa forodha yameongezeka kwa asilimia 18 kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia wastani wa Shilingi Trilioni 1.


"Mchango Katika Makusanyo ya Mapato ya Nchi Bandari ni lango kuu la Biashara za Kimataifa kati ya nchi ya Tanzania na nchi mbalimbali zinazo hudumiwa na Bandari za Tanzania. Bandari ya Dar es salaam inahudumia zaidi ya asilimia 95 ya Shehena zote zinazo pitia katika Bandari za Tanzania kwenda nchi jirani na hivyo kuchangia kiasi kikubwa katika makusanyo ya Kodi na Mapato mengine yasiyo ya kodi (kupitia Tozo) kwa Taifa. 

Nikitolea mfano wa Bandari ya Dar es salaam kuna Taasisi Zaidi ya 30 za umma (Mfano;TASAC, TPA, TRA, TRC, TAZARA, TBS, MKEMIA MKUU WA SERIKALI, POLISI, AFYA, UHAMIAJI, MISITU, KILIMO, MIFUGO, TAEC n.k) zinazotoa huduma mbalimbali ndani ya Bandari, mbali  na wadau wengine  toka Taasisi  binafsi na huduma hizi hulipiwa tozo na hivyo huwa ni vyanzo vya mapato kwa Taasisi zenyewe na Taifa kwa ujumla. Kwa mfano Mapato yaliyo kusanywa na TPA tu kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Juni, 2024) yamefikia Shilingi Trilioni 1.4, na kulingana na taarifa mbalimbali za kiuchumi, mchango wa sekta ya Bandari katika mapato yanayo kusanywa na TRA umeendelea kuwa kati ya asilimia 38-40 ya mapato yote yanayo kusanywa. Aidha, kwa mujibu wa taarifa za TRA, Mapato yatokanayo na ushuru wa forodha yameongezeka kwa asilimia 18 kutoka wastani wa Shilingi Bilioni 850 kwa  mwezi  hadi kufikia wastani wa Shilingi Trilioni 1".


Hadi sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) inasimamia Bandari rasmi 131 zilizoko katika Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu ambapo katika Bahari ya Hindi kuna bandari 32 na katika Maziwa Makuu kuna bandari 99.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bwana Plasduce Mbossa akifafanua jambo katika mkutano huo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la utangulizi alipokuwa akimkaribisha Mkurugenzi huyo wa TPA, Mbossa kuzungumza na wanahabari.

Waandishi wa habari wakiwajibika.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 5 YA KILA MWANANDOA KUFAHAMU