Wachezaji wa klabu ya Mashujaa FC wameahidiwa kitita cha Tsh 50 milioni endapo wataibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa CCM Lake Tanganyika, Kigoma.
Aidha, iwapo Mashujaa watatoka sare na Yanga, wachezaji hao watajipatia Tsh 25 milioni kama motisha kwa matokeo hayo.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na wa kusisimua, huku Mashujaa wakipania kuibuka na matokeo mazuri dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo.
Comments