UMEME MUSOMA VIJIJINI: MIRADI YA KUUNGANISHA VITONGOJI VYETU INAENDELEA

Kazi zilizokamilishwa:
1. Umeme Vijijini (Vijiji 68) -

Vijiji vyetu vyote 68 vimeunganishiwa umeme, yaani miundombinu ya usambazaji wa umeme imewekwa kwenye kila kijiji cha Jimboni mwetu

Hiyo ni sawa na asilimia 100 (100%) kwa upande wa vijiji vya Jimboni mwetu

2. Umeme kwenye Vitongoji 374

2a: Vitongoji 274 vimeunganishiwa umeme, hiyo ni sawa na asilimia 73.26 (73.26%) ya vitongoji vyetu vyote 374.

Kazi zinazoendelea kwa sasa (Bajeti 2024/25), na muda wa kukamilishwa kwake:

Mkandarasi I: Vitongoji 59 +10
Mradi utakamilika kabla ya tarehe 16 Nov 2025

Mkandarasi  II: Vitongoji 15
Mradi utakamilika ndani ya mwaka huu, 2025

2b: Vitongoji 100 vilivyosalia

Bajeti ya 2025/26 inayotayarishwa:
Vitongoji 50 vitaunganishiwa umeme

2c. Vitongoji 50 vinavyosalia:
Uunganishwaji wa umeme kwenye hivyo vitongoji 50 utakamilishwa kwa kutumia Bajeti ya Mwaka 2026/27 au kwa kutumia fedha zitakazopatikana kabla ya Bajeti ya 2025/26 kukamilika.

Taarifa hiyo hapo juu:
Kutoka: REA
Kwenda: Mbunge wa Jimbo

PONGEZI KWA SERIKALI YETU:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kumpongeza Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa michango mikubwa ya utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo ikiwemo ya usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyetu 68 vyenye jumla ya vitongoji 374 - ahsante sana!

REA: hongereni kwa kazi nzuri!

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

P. Box 6
Musoma



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 5 YA KILA MWANANDOA KUFAHAMU