BARAZA LA WANAWAKE UWEZESHAJI KIUCHUMI LAMPONGEZA RAIS SAMIA

 Na Mwandishi  Wetu


JUKWAA la Uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa wa Dodoma limetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupitishwa na mkutano  mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa na kusema watamuunga mkono kufanikisha anapata miaka mingine mitano ya kuongoza nchi. 

Pia jukwaa hilo limempingeza Dk Emmanuel  Nchimbi kwa kupitishwa kuwa mgombea mwenza wa nafasi ya Urais. 

Akitoa tamko hilo leo  Februari 26 2025 Jijini Dodoma,   Mwenyekiti wa Jukwaa  hilo Maryrobbi Mabhaya alisema  kuwa viongozi na wajumbe wa jukwaa wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwani ameweza kusimamia suala la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa kupitisha kanuni ya kusimamia mamlaka ya serikali za mitaa kuanzisha mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi unaotokana na mapato ya asilimia 10 ya mapato ndani ya halmashauri hivyo kuwezesha  upatikanaji wa mitaji kwa masharti nafuu kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

"Kuongezeka kwa fedha  za mikopo ya wanawake,vijana na wenye ulemavu  (asilimia 10)Kutoka Sh bilioni 2.5 mwaka 2021/2022 hadi kufikia Sh bilioni 3.3 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 32,ongezeko hilo limesaidia  kuongeza idadi ya vikundi Vinavyonufaika na mikopo inayotokana na halmashauri, "alisema. 

Pia alisema Rais Samia amewezesha makundi maalum ya watu maskini  kupitia mpango TASAF kuweza kujikimu, kupeleka watoto shake, kupata matibabu, kuanzisha miradi ya kujikwamua kwenye umaskini

Alitaja mambo mengine yaliyofanywa  ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo Ikiwemo ujenzi na ukarabati wa barabara za mijini na vijijini uliorahisisha kufikika kirahisi misimu yote ya mwaka. 

Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)  unerahisisha  mawasiliano kati ya Dodoma na Dar es Salaam na kuwezesha wafanyabiashara kuwa na safari za kwenda na kurudi. 

"Kujenga kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Msalato na kuboresha kiwanja cha ndege cha Dodoma na kuwezesha ndege kutua usiku ,"alisema

Aidha kuanzisha Samia legal aid ambayo inasaidia kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanyonge kutatuliwa migogoro kama ya mirathi na haki nyingine za wanawake. 

"Rais Samia amewezesha kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya na huduma za mama na mtoto, wanawake sasa wana uhakika wa uzazi salama, ameboresha miundombinu ya elimu kuanzia ngazi za shule ya msingi ,Sekondari,, vyuo vya kati na vyuo vikuu, "alisema. 

Mabhaya alisema Rais Samia amewezesha  kujenga tabia ya kuvumiliana na kusameheana, kupitia kukaribisha mashauriano na maridhiano ya makundi mbalimbali na kufanya nchi kuwa tulivu. 

"Jukwaa limeunganisha nguvu za makundi yote kumuunga mkono mama kufanikisha mitano tena, "alisema


Naye Mwajabu Nyamkomolo kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma,aliwataka wanawake kujiandaa kushiriki kongamano la wanawake kwa ajili ya maandalizi ya siku ya wanawake duniani iliopangwa kufanyika kitaifa Machi 8 jijini Arusha 


Aliwataka Jukwaa hilo kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kijamii yanayosaidia kuchagiza maendeleo yanayofanywa katika maeneo mbalimbali.


Aidha alisema serikali iko pamoja na jukwaa hilo,hivyo wanapaswa kujadili kwa kina mikakati yao waliojiwekea kwa ajili ya jukwaa hilo kupiga hatua moja mbele.







Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

MAMBO 8 MWANAMKE HUFANYA KWA MWANAUME ANAYEMPENDA