Bunge la Ubelgiji limeidhinisha azimio la kutaka kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Kijeshi dhidi ya Rwanda kutokana na mchango wake katika mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Azimio hilo la kurasa 11 liliwasilishwa na Mutyebere Ngoi, Mbunge wa Ubelgiji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutoka Chama cha Kisoshalisti. Iliidhinishwa na Wabunge wote wa bunge la Ubelgiji.
Katika rasimu hii ya azimio linalojulikana kama la 76, Wabunge wa Ubelgiji wanatoa wito mahsusi wa kusitishwa kwa mkataba wa ushirikiano wa Rwanda na Ubelgiji uliotiwa saini tarehe 19 Februari 2024. Pia inataka kukomeshwa kwa ushirikiano wa kijeshi na Rwanda. Azimio hilo pia linataka kuwekewa vikwazo vya kupiga marufuku uuzaji nje wa bidhaa za mafuta nchini Rwanda na vikwazo vingine dhidi ya viongozi wa wanamgambo wa M23.
Comments