Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa imeweka mkakati wa kuanzisha matibabu bingwa maalum kwa ajili ya wazee ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za afya za kibingwa zinazolikabili kundi hilo.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali hiyo, Prof. Abel Makubi ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma Machi 4, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
muelekeo na mafanikio ya miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Prof. Makubi
amesema kuwa kutokana na hospitali hiyo
kubobea kwenye aina mbalimbali za magonjwa na tafiti wamegundua kuwa kundi la
wazee ni miongoni mwa makundi yanayokumbwa na magonjwa hivyo umaalum wa matibabu na huduma za afya kiasi
cha kuhitaji kitengo maalum cha kibingwa .
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments