KAMWE OFISA HABARI WA 5 YANGA KUFUNGIWA


Habari zinasema ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amefungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kuchapisha habari zinazoushusha hadhi mchezo wa mpira wa miguu.
Kwa adhabu hiyo, Kamwe anakuwa ofisa habari wa tano wa klabu ya Yanga kuwahi kusimamishwa na TFF baada ya Jerry Muro, Hassan Bumbuli, Antonio Nuggaz na Haji Manara.
Hata hivyo, kamati ya maadili inatakiwa iishughulikie makosa ambayo yana uhusiano mdogo au hayana uhusiano kabisa na matukio ya uwanjani wakati Kamwe alizungumzia masuala yenye uhusiano moja kwa moja na kinachotokea uwanjani baada ya kuziomba mamlaka za soka zifanye uchunguzi dhidi ya uamuzi mbovu ambao mijadala ya vyombo vya habafi inasema unanufaisha timu moja.
 Na Angetile Osiah


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

MAMBO 8 MWANAMKE HUFANYA KWA MWANAUME ANAYEMPENDA