SERIKALI imesema itajenga Arena yenye uwezo wa kuingiza zaidi ya watu 15,000 katika eneo la Kawe Dar es Salaam. Kauli hiyo inakuja baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuharakisha ujenzi wa Arena ili wasanii wapate ukumbi wa kufanya shughuli zao. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema baada ya Rais Samia kufanya ziara Korea, amepata mkopo wa masharti nafuu wa Dola bilioni 2.5. Advertisement “Kati ya fedha hizo ameamua kukata Sh bilioni 450 kwa ajili ya kuzileta Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujenga Arena kwanza halafu itafuatia kijiji cha filamu,”amesema. Amesema fedha zitakapotoka Korea na kufika kwao wataanza ujenzi wa Arena mara moja ili uwanja huo uanze kutumika kwa ajili ya shughuli za michezo na burudani. “Arena inakuja, ndugu zangu wasanii tumshukuru sana Rais Samia, hili jambo lilikuwa linamu...
Comments