MUHIMBILI YAWEKEZA MITAMBO MIPYA YA KISASA

 

 Mkurugenzi wa Huduma za Upasiaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Rachel Mhavile akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Mohamed Janabi katika mkutano na vyombo vya habari katika Idara ya habari, jijini Dodoma Machi 6, 2025, kuelezea mafanikio ya hospitali hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hapa, Dkt. Mhavile akitaja baadhi ya mitambo ya kisasa iliyonunuliwa na MNH kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu.


Mtambo wa Angio-Suite

Serikali imenunua na kusimika mtambo wa kisasa (Angio-Suite) wa Tiba Radiolojia (Interventional Radiology) uliogharimu TZS. 2 Bil.ambao umewezesha hospitali kutoa matibabu ya ubingwa bobezi ambayo yalikuwa hayapatikani hapa nchini na kuongeza idadi ya aina za matibabu ya kibobezi katika eneo hilo ambapo takribani wagonjwa 2,300 wamehudumiwa tangu ulipofungwa mwaka 2022. Aidha, kupitia mtambo huo, kwa mara ya kwanza nchini, Hospitali imefanikiwa kuanzisha huduma mpya za kuweka mirija myembamba (catheters) kwa kutumia matundu madogo, kutoa damu iliyoganda katika mishipa ya damu na nyinginezo nyingi ambazo zinafanyika kwa ustadi wa hali ya juu.

 

2.5.2 Mashine Mpya ya Mammography

Aidha, Serikali ilinunua mashine mpya ya Mammography iliyogharimu TZS 1.8 Bi. ambayo ina uwezo wa kupima na kutoa picha zinazoweza kugundua uvimbe kwenye matiti ukiwa katika hatua za awali kabisa. Aidha jumla ya wagonjwa 810, wamehudumiwa kwa kutumia mashine hiyo tangu iliponunuliwa mwishoni mwa mwaka 2024. Mashine hii ambayo ni kisasa na pekee kwa hospitali za umma, inatumiwa na madaktari wabobezi wa radiolojia ya wanawake imeleta mapinduzi ya utoaji wa huduma za uchunguzi wa kisasa kwa wenye magonjwa ya matiti nchini.

 

2.5.3 Mashine Mpya ta CT-Scan

Serikali imeongeza mashine moja ya CT-Scan (dual) iliyogharimu TZS. 1.8 Bil. yenye uwezo wa vipande 128 hivyo kuongeza idadi ya wagonjwa wanaopimwa kwa siku kutoka 20 hadi zaidi ya 50 na majibu kupatikana kwa haraka, kumwezesha daktari kufanya maamuzi mapema na wagonjwa kupata matibabu stahiki kwa wakati.

 

2.5.4 Mashine Mpya ya MRI

Aidha, katika kipindi hichohicho, Serikali imeongeza mashine moja ya MRI yenye nguvu sumaku ya 1.5T ambayo inaweza kuona uvimbe mdogo kabisa… katika kupiga picha za uchunguzi iliyogharimu TZS. 2.6 Bil. hivyo kuondoa muda wa mgonjwa kusubiri kati ya siku haya ni mafanikio makubwa katika kuboresha huduma za matibabu nchini.

 

2.5.4 Mashine ya Kidigitali ya X-Ray iliyogharimu kiasi cha TZS. 358 Mil. ambapo kutokana na uwekezaji huo, Hospitali imefanikiwa kupunguza muda wa kutoa majibu ya radiolojia (turn-around time) kutoka saa 48 hadi 24 tangu mgonjwa anapopima.

 

2.5.5 Vifaa vingine

Hospitali ilifanikiwa kununua vifaa vingine vingi ikiwemo mashine za kusaidia wagonjwa kupumua 18 zilizogharimu kiasi cha TZS. 932 Mil, mashine za endoskopia zilizogharimu TZS. 215 n.k.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

MAMBO 8 MWANAMKE HUFANYA KWA MWANAUME ANAYEMPENDA