*•Asaini Kanuni za Fao la Utengamao ( Rehabilitation Benefits)*
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza Kwa vitendo dhamira yake ya kuwalinda wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika maendeleo ya Nchi yetu.
Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Machi 4, 2025 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko huo tangu kuanzishwa kwakwe, ikiwa ni hatua kubwa katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na familia zao.
Amesema WCF imeongeza wigo wa mafao ambapo hadi sasa unatoa jumla ya mafao saba ikiwemo Fao la Matibabu yasiyo na kikomo, Fao la Ulemavu wa Muda Mfupi, Fao la Ulemavu wa Kudumu, Fao la pensheni kwa wategemezi, Fao la Wasaidizi wa Mgonjwa, Fao la Utengamao, na Fao la Msaada wa Mazishi.
Pia, imeboresha mifumo ya ushughulikiaji wa fidia kwa wafanyakazi kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya huduma zinazotolewa na zinapatikana Mtandaoni, hali ambayo imeongeza ufanisi na tija katika utendajikazi wa Mfuko.
Vile vile, Kutoa elimu na uhamasishaji kwa waajiri na wafanyakazi kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi na usalama kazini, hivyo wafanyakazi wengi kuelewa haki zao pale wanapopata ugonjwa, ajali zinazotokana na kazi zao.
Katika Hatua nyengine , Waziri Kikwete amesaini Kanuni zinazoanzisha fao jipya la Utengamao linalolenga kumsaidia kumrudisha mfanyakazi aliyeumia kazini katika hali ya kuweza kuzalisha na kuendeleza msingi bora wa Maisha.
Waziri Kikwete , ameishukuru menejimenti ya WCF kwa kuishi maono ya Rais Samia ambapo wanawahakikishia Watanzania kuendelea na uzalishaji hata baada ya kuumia kazini.
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema WCF imepewa Cheti cha ithibati katika utoaji wa huduma bora kwa viwango vya Kim.
*
.
Comments