Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika kuanzia Septemba 10, 2025. Matokeo hayo yametangazwa leo, Jumatano Novemba 5, 2023, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said
Ally Mohamed.
Jumla ya watahiniwa 1,172,279 walishiriki katika mtihani huo, ambapo wavulana walikuwa 535,138 sawa na asilimia 45.65, na wasichana 637,141 sawa na
asilimia 54.35. Kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025 kimepanda kwa asilimia 0.93.
Watahiniwa 937,581, ambao ni asilimia 81.80 ya 1,146,164 waliofanya mtihani, wamepata madaraja ya
A, B na C. Takwimu hizo zinaonesha ongezeko la ufaulu ukilinganisha na mwaka 2024, ambapo asilimia ya waliofaulu ilikuwa 80.87.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kati ya waliofaulu, wavulana ni 429,104 sawa na asilimia 82.51, na wasichana ni 508,477 sawa na asilimia 81.21.
Pia, NECTA imeeleza kuwa ubora wa matokeo nao umeongezeka. Watahiniwa 422,923 sawa na asilimia
36.90 wamepata madaraja ya juu (A na B), ikilinganishwa na asilimia 35.83 mwaka 2024, hivyo kuonyesha ongezeko la asilimia 1.07.

Comments