MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

 AGE - 49 years


✍️🏽Falsafa ya Msingi ya Uchezaji

Ni kocha anayeamini katika mpira wa akili(Intelligent Football) usiotegemea nguvu au kasi tu bali ufahamu wa nafasi, mpangilio na uamuzi wa haraka wa matukio.

🎨 Mambo Makuu ya Falsafa yake


Kushambulia kwa mpangilio mzuri, kujenga mashambulizi kupitia pasi fupi na kutumia wachezaji wa pembeni kufanya quick transition.


Hapendi timu yake imiliki kwa takwimu tu bali kwa kutengeneza nafasi za maana na kimkakati.


Timu zake zina uwezo mkubwa wa kugeuka kutoka kulinda hadi kushambulia ndani ya sekunde chache.


Timu iikiwa inazuia wachezaji wake wote wanashiriki kujilinda hata washambuliaji wana jukumu la kurudi nyuma pale wakati hawana mpira


Hataki timu yake icheze kwa vurugu ili kushinda haraka bali kwa mpangilio na kujenga utambulisho wao wa kudumu.

✍️🏽Mifumo ya Uchezaji Anayopendelea(Favorite Formations)

Pedro Gonçalves si kocha anayeshikilia mfumo mmoja pekee yaani “dogmatic”, Anapendelea sana mifumo mitatu.

🎨 4-2-3-1

Huu ulikuwa Mfumo wake maarufu akiwa Angola ambao lengo lake ni kutoa usawa kati ya kuzuia na kushambulia kwa kutumia viungo na washambuliaji wa pembeni.

🎨 4-3-3

Anautumia dhidi ya wapinzani wanaocheza wanaokabia sana juu ili kutoa machaguo mengi zaidi ya pasi na mapana ya uwanja kutoka nyuma kwenda mbele.


Huu anatumia mara nyingi wakati anataka kushambulia kwa tahadhari na kulinda matokeo zaidi. Pia anabadilika muundo na majukumu ya wachezaji kulingana na mwenendo wa mechi.

✍️🏽Vitu gani natarajia kuona akiongeza Young Africans? 🔰

1-Mabadiliko ya muundo wa ushambuliaji wenye mpangilio mzuri kutoka chini

2-Kuimarika kwa muundo wa uzuiaji kitu kinachoweza kuwalipa kwenye mechi kubwa zneye presha hasa za CAF CL.

3-Kuinua ubora kwa baadhi ya Wachezaji wa Young Africans.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

RAIS SAMIA AMZAWADIA NYUMBA SIMBU

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA