Ni nadra sana kusikia watoto wa Viongozi wakuu wa nchi hasa Rais hawajulikani, lakini Wakati wa Utawala wa Dkt John Magufuli Hilo liliwezekana aliiweka mbali sana familia yake na serikali, vyombo vya Habari na hata masikioni mwa watu.
Katika kipindi chote Cha utawala wa Rais wa awamu ya Tano Dkt Magufuli, wengi walikosa kujua mengi kuhusu familia yake, jambo lililowafanya kuwa na faragha sana. Hata hivyo, kwenye mazishi ya kitaifa jijini Dodoma,2021 siri hizi zilifichuka.
kwenye mazishi ya kitaifa jijini Dodoma, familia yake ilijulikana kuwa Dkt Magufuli ameacha watoto saba na wajukuu 10.
Waziri Profesa Palamagamba Kabudi ambaye ndiye Alisoma wasifu huo wa JPM Alitaja watoto hao ni Suzzan John Magufuli, Edna John Magufuli, Joseph John Magufuli (pichani), Jesca John Magufuli, Ruth John Magufuli, Jurgen John Magufuli, Jeremiah John Magufuli na Juliana John Magufuli aliyefariki dunia wakati baba yake akiwa waziri.
Jina maarufu kwa Watanzania mpaka Leo na wengi walimfahamu mwanaye tangu kipindi hicho akiwa madarakani lilikuwa ni Jesca Magufuli ambaye inaelezwa alisoma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Profesa Kabudi kwenye mazishi hayo alisema Rais Magufuli alifunga ndoa mwaka 1989 na Janeth Mathias Mbizo. na mwenyewe Dkt Magufuli aliwahi kueleza kuhusu ndoa yake wakati akiwa kwenye mdahalo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwamba haikuwa na shamra shamra.
"Siku niliyooa watu wengi hawakujua...na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana.
"Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padri, tena zilikuwa za shaba. Padri pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunywa pepsi na mke wangu alikunywa mirinda...Baada ya hapo nikaenda zangu lab (maabara) kuendelea na shughuli zangu."
Padri aliyewafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwa mujibu wa Rais Magufuli anaitwa Msemwa na sasa yupo Tanga. "Mfuateni Father (Padri) Msemwa yeye atawaeleza vizuri zaidi." Alisema JPM
Magufuli pia alisema hata ndoa za watoto Wake huwa haziambatani na sherehe kubwa. "Mpaka sasa watoto zangu watatu wameshafunga ndoa" Alisema JPM
Umejifunza nini kutoka Kwa Hayati Dkt Magufuli ✍️
Rest in peace JPM 🕊️ đź’”
Ameandika: Mudumoh

Comments