Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Besigye

Image copyrightAP
Image captionDkt Besigye amekamatwa akielekea makao makuu ya Tume ya Uchaguzi
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi.
Watu walioshuhudia wanasema amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.
Besigye
Image captionBesigye alizuiliwa na polisi mara tatu wiki iliyopita
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.
PolisiImage copyrightAFP
Image captionPolisi walivamia afisi za chama cha FDC Ijumaa wiki iliyopita
Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki iliyopita.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Wasifu wa Kizza Besigye

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI